Bodi ya REA yaagwa na kutunukiwa TUZO kwa utumishi wenye tija

NA VERONICA SIMBA-REA

BODI ya Nishati Vijijini inayosimamia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), imehitimisha muda wake kisheria na kupongezwa kwa kutekeleza majukumu yake kwa juhudi, weledi, uadilifu na uzalendo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali (kushoto) akipokea Taarifa ya Utendaji Kazi wa Bodi ya Nishati Vijijini iliyohitimisha muda wake kisheria Januari 31, 2022 kutoka kwa Mwenyekiti wake, Wakili Julius Kalolo. (Picha na Veronica Simba-REA).

Akizungumza mwishoni mwa wiki katika hafla fupi ya kuwaaga wajumbe wa bodi hiyo, mgeni rasmi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali aliwaeleza kuwa Serikali inatambua mchango wao katika majukumu mbalimbali waliyotekeleza, hususani katika kuongeza hali ya upatikanaji umeme vijijini hadi kufikia asilimia 69.8.

Mahimbali ambaye alimwakilisha Waziri wa Nishati, alieleza majukumu mengine yaliyotekelezwa na Bodi hiyo kwa ufanisi mkubwa ni pamoja na kuongezeka uunganishaji umeme kwa wateja wa vijijini kutoka 584,639 hadi kufikia wateja 956,511 sawa na asilimia 63.6. 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali (katikati –waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini iliyohitimisha muda wake kisheria Januari 31, 2022. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi Wakili Julius Kalolo na kulia ni Katibu wa Bodi ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy. (Picha na Veronica Simba-REA).

Alitaja mafanikio mengine kuwa ni kusimamia kuongezeka kwa Mfuko wa Nishati Vijijini kutoka Shilingi Bilioni 1,337 hadi Bilioni 1,684 sawa na asilimia 26. 

Aidha, kuongezeka kwa michango ya wabia wa maendeleo kutoka Shilingi Bilioni 252 hadi Bilioni 560 sawa na asilimia 123 pamoja na kusimamia kikamilifu maslahi ya wafanyakazi wa Wakala.

Naibu Katibu Mkuu alieleza zaidi kuwa, Bodi ilisimamia kikamilifu utekelezaji wa jukumu la msingi la Wakala ambalo ni kuhamasisha na kuwezesha upatikanaji wa nishati bora vijijini ili kuboresha maisha ya wananchi waishio vijijini, kiuchumi na kijamii kupitia upatikanaji wa nishati hiyo, hivyo kuifanya Serikali kutembea kifua mbele kwa mafanikio yaliyopatikana ambayo yameacha alama Tanzania na Afrika nzima. 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuwaaga na kuwatunuku tuzo Wajumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini iliyohitimisha muda wake kisheria. (Picha na Veronica Simba-REA).
Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini, Wakili Julius Kalolo akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuwaaga na kuwatunuku tuzo Wajumbe wa Bodi hiyo ambayo imehitimisha muda wake kisheria Januari 31, 2022. Mgeni Rasmi katika hafla hiyo alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali ambaye alimwakilisha Waziri wa Nishati.(Picha na Veronica Simba-REA).

“Kwa niaba ya Serikali, ninawashukuru kwa kusimamia utekelezaji wa Sera ya Nishati Vijijini kwa uadilifu mkubwa na maslahi mapana ya Taifa. Kwa hakika, kazi hii ni ngumu na inahitaji watu wenye uadilifu na uzalendo wa hali ya juu kutekeleza majukumu haya kama mlivyofanya ninyi,”amesema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi, Wakili Julius Kalolo, alitoa shukrani kwa Serikali, Wabia wa Maendeleo, Wizara ya Nishati, Menejimenti na Wafanyakazi wote wa REA, kwa ushirikiano wa hali na mali katika kuiwezesha Bodi kutekeleza majukumu yake kikamilifu.

Wakili Kalolo alifafanua kuwa, kitendo cha Serikali na Wabia wa Maendeleo kuendelea kutoa fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi ya nishati vijijini kimeiwezesha Bodi hiyo kupata mafanikio yote iliyofikia. 
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Hassan Saidy akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuwaaga na kuwatunuku tuzo Wajumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB) ambayo imehitimisha muda wake kisheria Januari 31, 2022. Mgeni Rasmi katika hafla hiyo alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali ambaye alimwakilisha Waziri wa Nishati. (Picha na Veronica Simba-REA). 
Mjumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini, Dailin Mghweno (kushoto) akipokea Tuzo ya kutambua mchango wake katika sekta ya nishati vijijini kutoka kwa Mgeni Rasmi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali wakati wa hafla fupi ya kuwaaga na kuwatunuku tuzo Wajumbe wa Bodi hiyo ambayo imehitimisha muda wake kisheria Januari 31, 2022. (Picha na Veronica Simba-REA).

Aidha, alisema kuwa ushirikiano uliotolewa na wafanyakazi wote wa REA, Wizara na Taasisi mbalimbali zinazohusiana na Wakala huo, umechangia kwa kiasi kikubwa kufikia mafanikio hayo.

Akitoa salamu za shukrani kwa niaba ya Wajumbe wenzake wa Bodi, Mkurugenzi Dailin Mghweno alitoa shukrani kwa Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kuwaamini na kuendelea kuwapa nafasi ya kuwatumikia Watanzania hadi walipohitimisha muda wao.
Mjumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini, Louis Accaro (kushoto) akipokea Tuzo ya kutambua mchango wake katika sekta ya nishati vijijini kutoka kwa Mgeni Rasmi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali wakati wa hafla fupi ya kuwaaga na kuwatunuku tuzo Wajumbe wa Bodi hiyo ambayo imehitimisha muda wake kisheria Januari 31, 2022. (Picha na Veronica Simba-REA).
Mjumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini, Mhandisi Styden Rwebangila (kushoto) akipokea Cheti Maalum cha kutambua mchango wake katika sekta ya nishati vijijini kutoka kwa Mgeni Rasmi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali wakati wa hafla fupi ya kuwaaga na kuwatunuku tuzo Wajumbe wa Bodi hiyo ambayo imehitimisha muda wake kisheria Januari 31, 2022. (Picha na Veronica Simba-REA).

Naye Mkurugenzi Mhandisi Francis Songela aliahidi kuwa Wajumbe wote wa Bodi hiyo wataendelea kutoa ushirikiano kwa REA na Serikali kwa ujumla katika kuhakikisha malengo yote yaliyopangwa kutekelezwa yanafikiwa.

“Tutaendelea kuwa Mabalozi wazuri na tuko tayari muda wote kutoa ushirikiano pale utakapohitajika,” alisisitiza Mhandisi Songela.

Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy aliielezea Bodi hiyo kuwa ya kipekee kutokana na kuwa yenye ushirikiano mkubwa kwa Wakala. 
Mjumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini, Florian Haule (kushoto) akipokea Tuzo ya kutambua mchango wake katika sekta ya nishati vijijini kutoka kwa Mgeni Rasmi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali wakati wa hafla fupi ya kuwaaga na kuwatunuku tuzo Wajumbe wa Bodi hiyo ambayo imehitimisha muda wake kisheria Januari 31, 2022. (Picha na Veronica Simba-REA).
Mjumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini, CPA Oswald Urassa (kushoto) akipokea Cheti Maalum cha kutambua mchango wake katika sekta ya nishati vijijini kutoka kwa Mgeni Rasmi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali wakati wa hafla fupi ya kuwaaga na kuwatunuku tuzo Wajumbe wa Bodi hiyo ambayo imehitimisha muda wake kisheria Januari 31, 2022. (Picha na Veronica Simba-REA).
Mjumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini, Mhandisi Francis Songela (kushoto) akipokea Cheti Maalum cha kutambua mchango wake katika sekta ya nishati vijijini kutoka kwa Mgeni Rasmi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali wakati wa hafla fupi ya kuwaaga na kuwatunuku tuzo Wajumbe wa Bodi hiyo ambayo imehitimisha muda wake kisheria Januari 31, 2022.(Picha na Veronica Simba-REA).
Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini, Wakili Julius Kalolo (kushoto) akipokea Cheti Maalum cha kutambua mchango wake katika sekta ya nishati vijijini kutoka kwa Mgeni Rasmi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali wakati wa hafla fupi ya kuwaaga na kuwatunuku tuzo Wajumbe wa Bodi hiyo ambayo imehitimisha muda wake kisheria Januari 31, 2022. (Picha na Veronica Simba-REA).
Katibu wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB) ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy (kushoto) akipokea Tuzo ya kutambua mchango wake katika sekta ya nishati vijijini kutoka kwa Mgeni Rasmi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali wakati wa hafla fupi ya kuwaaga na kuwatunuku tuzo Wajumbe wa Bodi hiyo ambayo imehitimisha muda wake kisheria Januari 31, 2022. (Picha na Veronica Simba-REA).
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali (katikati –waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini iliyohitimisha muda wake kisheria Januari 31, 2022 (waliokaa) pamoja na baadhi ya Wafanyakazi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA). Kulia kwa Naibu Katibu Mkuu ni Mwenyekiti wa Bodi, Wakili Julius Kalolo na kushoto kwake ni Katibu wa Bodi ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy.

"Kwakuwa wanatoka sehemu mbalimbali, kila mmoja ametumia ujuzi na uzoefu wake kuhakikisha REA inasonga mbele zaidi na zaidi. 

Katika hafla hiyo, Mgeni Rasmi aliwatunuku tuzo na vyeti maalum kama ishara ya kutambua utumishi wao uliotukuka ambao umeleta tija katika sekta ya nishati vijijini.

Wajumbe wa Bodi hiyo iliyoteuliwa Januari 31, 2019 na ambayo imehitimisha muda wake wa miaka mitatu kisheria ni Mhandisi Styden Rwebangila akiwakilisha

Wizara ya Nishati, Dailin Mgweno (Umoja wa Walaji Tanzania), Mhandisi Francis Songela (Wabia wa Maendeleo), Louis Accaro (Sekta Binafsi), Frolian Haule (Vyama vya Ushirika) na CPA Oswald Urassa (Umoja wa Benki Tanzania).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news