NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Bw. Atupele Mwambene ametoa wito kwa walimu walioshiriki mafunzo ya somo la Elimu ya Biashara kuonesha ushirikiano kwa walimu wataowakuta katika vituo vyao vya kazi ili kuwasaidia watoto katika malezi pamoja na ujifunzaji.
Ametoa wito huo Agosti 21, 2026 wakati akihitimisha mafunzo ya somo la Elimu ya Biashara kwa walimu wa kujitolea waliofadhliwa na Shirika lisilo la kiserikali la EDUCATE, tukio lililofanyika katika ukumbi wa Nkurumah chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Bw. Mwambene amesema, ili kufikia malengo ya kuboresha elimu katika mazingira mtayoenda msisite kuomba ushauri na miongozo ya kiutendaji kwa viongozi na wenyeji mtakaowakuta jambo litaloimarisha upendo na ushirikiano katika kutimiza wajibu wa malezi na ufundishaji kwa wanafunzi.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo






















