Magazeti leo Agosti 24,2026

Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) umeendelea kutoa mafunzo maalum ya siku mbili kuhusu Uongozi na Usimamizi wa Utekelezaji wa Mtaala Ulioboreshwa, yakilenga kuimarisha uwezo wa Wakuu wa Shule za Sekondari katika kusimamia kwa ufanisi mabadiliko ya mtaala.







Mafunzo hayo yameanza tarehe 24 na yatahitimishwa tarehe 25 Agosti 2026 katika Kampasi ya ADEM Bagamoyo, yamewashirikisha Wakuu wa Shule za Sekondari 163 kutoka Mkoa wa Ruvuma na yamefadhiliwa na Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA).

Katika mafunzo hayo, washiriki watajadili mada mbalimbali zinazolenga kuwajengea uwezo katika maeneo muhimu ya Uongozi na Usimamizi wa Shule, ikiwemo Uongozi na Usimamizi wa Shule, Usimamizi wa Utekelezaji wa Mtaala, Uchambuzi wa Mtaala Ulioboreshwa, Maadili na Itifaki pamoja na Huduma kwa Wateja.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here