Clatous Chama arejea Simba SC

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

KLABU ya Simba imetangaza kurejea tena kikosini kwa Kiungo mshambuliaji kutoka Zambia, Clatous Chama akitokea RS Berkane ya Morocco alikokwenda huko miezi mitano iliyopita.
Chama alijiunga na Simba mwaka 2018 na kuondoka mwaka 2021 kabla ya kurejea Simba na kutambulishwa rasmi leo.

Kupitia bango kubwa lililotolewa na Simba likiwa na picha ya Chama limesomeka kwa,“Karibu nyumbani, Welcome home” .

Mshambuliaji huyo aliondoka Simba SC Agosti 13, 2021 na kujiunga na Klabu ya RS Berkane ya Morocco na sasa anarejea baada ya kudaiwa kushindwa kuzoea mazingira nchini Morocco.

Post a Comment

0 Comments