Mathayo Cup yawajaza vijana fedha ng'ombe, mbuzi Musoma Mjini

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

UBUNIFU wa Mbunge wa Musoma Mjini mkoani Mara, Mheshimiwa Vedastus Mathayo Manyinyi katika sekta ya michezo umetajwa kuwa moja wapo ya njia inayowaleta pamoja vijana, kuwapa mawazo ya kufikiri mambo mapya kwa ajili ya maendeleo yao na Taifa.
Sambamba na kuimarisha umoja, mshikamano, upendo, amani ambazo ni miongoni mwa nguzo muhimu katika kuzifikia ndoto zao mjini Musoma.

Hayo yamebainishwa kwa nyakati tofauti na vijana ambao wamempongeza Mbunge huyo wakati wakizungumza na DIRAMAKINI BLOG kuelezea namna ambavyo Kombe la Mbunge Mathyo (Mathayo Cup -Barabarani 2022) lilivyowapa maono mapya katika kuzifikia ndoto zao.

"Tunampongeza sana Mheshimiwa Mbunge Vedastus Mathayo Manyinyi kwa ubunifu huu, hili ni kati ya makombe ambayo yanawakutanisha vijana wa rika tofauti na kudumisha umoja, upendo na mshikamano, tumeona kadri tunavyoshiriki katika michezo fahamu zetu zinapanuka na kuwa na mawazo mapya kwa ajili ya kufikiri mambo mema zaidi kwa ajili ya maendeleo yetu, jamii na Taifa kwa ujumla,"amesema mmoja wa vijana ambao walikuwa wakifuatilia michuano hiyo.
Aidha, baada ya michuano ya Mathayo Cup ambayo imedumu tangu mwishoni mwa mwaka jana ikizishirikisha timu kadhaa imefikia tamati huku washindi wakipatiwa zawadi mbalimbali.

Ni wakati wa fainali ambayo imefanyiki leo Januari 16, 2022 mjini Musoma ambapo Mhe.Patrick William Gumbo ambaye ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Musoma Mjini amemwakilisha Mhe.Vedastus Mathayo kwenye fainali hizo.
Mshatiki Meya huyo amekabidhi kombe na zawadi kwa washindi wakiwemo nafasi ya kwanza .Mshikamano Bodaboda ambao wametunukiwa fedha taslimu shilingi 500,000 na ng'ombe Mtamba.

Washindi wa pili ni Bweri Bodaboda ambao wamepatiwa fedha taslimu shilingi 400,000 na mbuzi huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Nyakato Bodaboda ambao wamezawadiwa shilingi 200,000 na mbuzi. 
Mhe.Mstahiki Meya amewapongeza vijana hao na kuwashukuru kwa namna walivyoshiriki kwenye kashindano hayo kwa nidhamu na weledi wa hali ya juu.
Sambamba na hayo amewapa salaamu kutoka kwa Mhe.Mbunge ambazo zimewataka kujiandaa vyema na mashindano yanayofuata kwa msimu wa 2022/2023. 


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news