Moshi mweupe Dodoma leo

NA MWANDISHI MAALUM

KIKAO cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kinafanyika leo Alhamisi Januari 20, 2022 baada ya kutofanyika Januari 18, 2022 kama ilivyokuwa imepangwa awali.
Kikao hi hicho cha leo ambacho kiftafanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM (White House jijini Dodoma, kitaendeshwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan. 

Kwa mujibu wa taarifa, kikao hicho kitatanguliwa na kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM chini ya Mwenyekiti wake Katibu Mkuu wa CCM,Daniel Chongolo.

Awali wana CCM 71 waliochukua fomu ya kuutaka uspika na 70 kufanikiwa kurejesha wanatarajiwa kujadiliwa ili kupata mwakilishi sahihi katika mhimili wa Serikali wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news