Mshirikina anayedaiwa kutengeneza radi na kumuua mwananchi mwenzake achomwa na kitu chenye ncha kali Katavi

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

MKAZI wa Kijiji cha Mtisi katika Halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi, Baraka Said (30) ameuawa na wananchi baada ya kukatwa na kitu chenye ncha kali kwenye paji la uso na kupigwa na kitu kizito kisogoni akituhumiwa kujihusisha na ushirikina wa kutengeneza radi.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi, Sylvester Ibrahimu amesema tukio hilo limetokea Januari 24, 2022 saa 12 jioni kijijini hapo.

Amesema, wananchi hao walimtuhumu marehemu kutengeneza radi iliyompiga Anjelina Revocatus (16) mkazi wa kijiji hicho na kusababisha kifo chake wakati anatibiwa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Katavi.

"Watuhumiwa nane wamekamatwa,John Mayonjuwa, Mashaka Mathias, Sele Richard, Revocatus Reymond, Julias Dalali, Hawa Rashid, Agnes Rashid na Tausi Abdu. Upelekezi ukikamilika watafikishwa mahakamani," amesema Ibrahimu.

Aidha,katika tukio lingine Ibrahimu amesema nyumba 10 zilizojengwa kwa miti na kuezekwa kwa nyasi kijiji cha Igongwe zimechomwa moto na kuteketeza mali zote zilizokuwa ndani.

Amesema, tukio hilo limefanywa na baadhi ya wananchi wa Stalike waliojichukulia sheria mkononi wakigombania mashamba kati yao na Kijiji cha Igongwe lililopelekea kifo cha Klisent Mwananjela (40) mkazi wa Kijiji cha Stalike.

Pia amesema, watu saba wamekamatwa wakituhumiwa kuhusika na tukio hilo la mauaji akiwamo Mtanda Yegela (19) mkazi wa Itenka A, Maico Kihongwe (48) mwenyekiti wa kijiji cha Muungano na Lucas Shabai (22) mkazi wa kijiji cha Mnyamasi.

Wengine ni James Charles (23) mkazi wa kijiji cha Itenka, Salula Tano (27) mkazi wa kijiji cha Itenka, Frederick Edward (26) mfanyabiashara wa Ubilimbi Kahama na Samwel Maico (44) mkazi wa Itenka.

"Watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani pindi upelelezi utakapokamilika kujibu tuhuma zinazowakabili na juhudi za kuwasaka wengine waliosababisha mauaji zinaendelea," amesema.

Mbali na hayo watuhumiwa wanane wamekamatwa kwa tuhuma za kuhusika na tukio la kuchoma moto nyumba 10 mali ya Sayi Wema mkazi wa Kijiji cha Igongwe.

"Walitekeleza nguo, mazao ya mahindi na mpunga thamani yake haijapatikana,tumewakamata Daud Gembe (54) mkazi wa kijiji cha Stalike,Abas John (30)mkazi wa kijiji cha Stalike,Genius Sindani (65)mkazi wa Stalike, Julia's Nicolaus (38) mkazi wa kijiji cha Stalike na Japhari Razaro (48) mkazi wa Vikonge.

"Godfrey Basili(44)mkazi wa Stalike,Joseph Leopard (33) mkazi wa Stalike na Klisent Mwananjela (40) mkazi wa Stalike,watuhumiwa wote wamefikishwa mahakama ya mkoa kujibu mashtaka hao,"amesema.

Wakati huo huo amewataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi kitendo kinachosababisha kujeruhi na mauaji katika jamii.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news