Ndoa ya Diamond na Zuchu yakaribia, Khadija Kopa afunguka

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

FUNUNU za muda mrefu katika mitandao ya kijamii huku ikipambwa na picha za matukio tofauti ambayo Diamond Platnumz ameongozana na Zuchu kuhusu uhusiano wa kimapenzi baina ya mastaa hao wawili huenda sasa zikarasimishwa rasmi na kuwa taarifa kamili. 
Ni baada ya ishara zote kuonesha kuwa, wawili hao sasa ni wapenzi na muda wowote wanatarajia kufunga ndoa.

Ukaribu wa Diamond na Zuchu ndio ulichochea gumzo na wadadisi wa mambo kuanza kuunganisha namba ili kupata picha kamili kama ni kweli wawili hao ni wapenzi au la!. 

Kwa mujibu wa taarifa iliyoifikia DIRAMAKINI BLOG ni kwamba, tangu WCB ilipomtangaza Zuchu kama msanii wao, Diamond alikuwa mstari wa mbele katika kumnadi mrembo huyo popote pale anapopata nafasi, iwe kwenye mitandao ya kijamii au kwenye mikutano ya kibiashara anayofanya na kampuni tofauti.

Kwa mfano ni Julai 18,2020 msanii Diamond alitangaza kuwa yupo singo na mashabiki wakae tayari kumuona mrembo wake mpya atakayepita naye kwenye ‘red carpet’ pale Mlimani City kwenye uzinduzi wa albamu fupi (EP), I Am Zuchu. 

Wengine walitarajia Diamond atapita kwenye zuria jekundu na warembo ambao wanafahamika na aliwahi kuwa nao kwenye uhusiano kama vile Zari The Boss Lady, Wema Sepetu, Hamissa Mobetto na wengineo lakini akawashangaza maahabiki kwa kuingia ukumbini na Zuchu yakiwemo matukio mengi yaliyofuata. Uhusiano wa Diamond na Zuchu unatajwa kuwa miongoni mwa vipaumbele muhimu kwa mastaa hao ndani ya mwaka huu.

Baraka za Mama

Leo, Januari 31, 2022 mama yake Zuchu, Khadija Kopa ametoa baraka ambazo wadadisi wa mambo wameunganisha taarifa na kupata matokeo kuwa, hizo ni baraka za wawili wapendanao baina ya Diamond na Zuchu.

"Zuhura mwanangu nimekulea kwenye maadili na najua wewe ni binti mwenye maamuzi sahihi na mimi kama Mama yako niseme sina budi kukusapoti.

"Tarehe 14 inaenda kua siku yako kubwa hakuna mwanamke asiye na ndoto hii.Mwenyenzi Mungu akakusimamie najua hutoniangusha. Siku hii isiwe tu siku yako kubwa duniani basi pia ikawe ndio mwanzo wa maisha mapya yenye furaha.Mwenyenzi Mungu akulinde kiziwanda changu Amin,"ameeleza Khadija Kopa katika ukurasa wake wa Instargram leo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news