RAIS DKT.MWINYI AONGOZA SHERERE ZA KILELE CHA MAADHIMISHO YA MIAKA 58 YA MAPINDUZI


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi akisalimia wananchi alipoingia katika Uwanja wa Amaan jijini Zanzibar kuongoza Sherehe za Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi akipokea salamu ya Heshima ya Gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama katika Uwanja wa Amaan jijini Zanzibar wakati wa Sherehe za kilele cha Maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo.
Mke wa Rais wa Zanzibar,Mama Mariam Mwinyi (katikati) Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Othman (kulia) Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Akson wakisimama wakati wa kupokea Salamu ya Heshma ya Gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama katika kilele cha Maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar hafla iliyofanyika leo katika Uwanja wa Amaan jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi akikagua Gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama katika Uwanja wa Amaan jijini Zanzibar wakati wa Sherehe za kilele cha Maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, leo. (Picha na Ikulu).

Post a Comment

0 Comments