Rais Dkt.Mwinyi awaapisha viongozi mbalimbali, ateta na wanahabari

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewaapisha watendaji mbalimbali aliowateua hivi karibuni kushika nyadhifa zao.

Hafla hiyo ya kiapo imefanyika Ikulu jijini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi wakuu wa Kitaifa, mawaziri, viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa dini pamoja na wanafamilia.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mheshimiwa Jaji Aziza Iddi Sued,kuwa Mwenyekiti wa Mahkama ya Rufaa ya Idara maalum ya SMZ, hafla hiyo iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha zote na Ikulu).

Viongozi walioapishwa kushika nyadhifa hizo ni pamoja na Jaji Aziza Idd Sued aliyeteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufaa ya Idara Maalum za SMZ pamoja na Dkt.Said Seif Mzee aliyeteuliwa kuwa Mhasibu Mkuu wa Serikali Zanzibar katika Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango.

Mwingine ni Rahma Salim Mahafoudh aliyeteuliwa kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar katika Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Dkt.Rahma Salim Mahfoudh kuwa Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar, Dkt. Rahma Salim Mahfoudh, hafla hiyo iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Dkt. Said Seif Mzee kuwa Mhasibu Mkuu wa Serikali Zanzibar katika Ofisi ya Rais,Fedha na Mipango,hafla hiyo iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe.Hemed Suleiman Abdulla, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Dkt.Mwinyi Talib Haji na Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Saleh Omar Kabi, wamehudhuria katika hafla kuapishwa viongozi walioteuliwa na Rais kushika nafasi mbalimbali katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar. 
Viongozi wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama Zanzibar waliohudhuria katika hafla kuapishwa Viongozi walioteuliwa na Rais kushika nafasi mbali mbali katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.31-01-2022, (Picha na Ikulu). 

Miongoni mwa viongozi waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, Kaimu Jaji Mkuu wa Zanzibar Khamis Ramadhan Abdalla, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Dkt.Mwinyi Talib Haji, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zena Ahmeid Said, Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Saleh Omar Kaab, mawaziri, wakuu wa vikosi vya ulinzi na usalama, viongozi wa vyama vya siasa pamoja na wanafamilia. 

Rais ateta na wanahabari

Wakati huo huo, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt.Hussein Ali Mwinyi amefanya mahojiano na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kusisitiza jambo wakati wa mkutano wake na wahariri wa vyombo vya habari na waandishi wa magazeti na TV, uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi, akifuatilia maswali ya wahariri wa vyombo vya habari na waandishi wa habari za magazeti na TV, kupitia njia ya zoom, wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika leo Januari 31,2022 katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar. 
Mwandishi mkongwe wa habari Zanzibar, Bw. Said Salim akiuliza swali wakati wa mkutano wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi na wahariri wa vyombo vya habari na waandishi wa habari wa magazeti na TV, uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar. 
Mhariri mwandamizi kutoka New Habari, Bw. Absalom Kibanda akiuliza swali wakati wa mkutano wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi na wahariri wa vyombo vya habari na waandishi wa habari wa magazeti na TV.
Wahariri wa vyombo vya habari na waandishi wa habari wa magazeti na TV, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akijibu maswali yalioulizwa wakati wa mkutano wake uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar leo.
Waandishi wa habari na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wa magazeti na TV wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani ) akizunguma katika mkutano wake uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar.

Katika hafla hiyo iliyofanyika Ikulu jijini Zanzibar, Dkt.Mwinyi alijibu maswali mbalimbali pamoja na kupokea ushauri kutoka kwa waandishi wa habari katika nyanja za siasa, uwekezaji, ustawi wa jamii, michezo, ulinzi na usalama.

Sambamba na kutoa rambirambi kwa waandishi wa habari watano waliofariki dunia mkoani Mwanza hivi karibuni.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news