Magazeti leo Juni 1,2026

Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Grace Magembe amewataka watumishi wa afya nchini kuwa makini zaidi katika kipindi hiki cha tahadhari ya ugonjwa wa Ebola, kufuatia mlipuko uliojitokeza katika nchi jirani za Congo na Uganda ili kujikinga wao na kuwakinga wengine.
Dkt. Magembe amesema hayo Mei 31, 2026 wakati akizungumza na watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera na Hospitali ya Manispaa ya Bukoba akihitimisha ziara yake ya kukagua hali ya utayari wa kujikinga na ugonjwa wa ebola usiingie nchini katika maeneo ya mipakani mkoani humo.

Dkt. Magembe amesema kuwa dalili za awali za Ebola kama homa, kuumwa kichwa, uchovu wa mwili, kutapika na kuharisha zinaweza kufanana na magonjwa mengine, hivyo wahudumu wa afya wanapaswa kuwa na umakini mkubwa wanapowahudumia wagonjwa na kuchukua tahadhari zote muhimu za kinga.
















Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here