Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Bw. Balandya Elikana amesema ajenda ya utunzaji na uhifadhi wa mazingira ni eneo la kipaumbele katika mipango ya maendeleo ya mkoa huo.

Bw. Elikana amesema hayo Mei 29, 2026 wakati wa mazungumzo baina na timu ya watalaamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais waliofika ofisini kwake kwa ajili ya kupokea taarifa ya maandalizi ya maadhimisho ya Siku Mazingira Duniani, 2026 katika Mkoa huo.
Elikana amesema Mkoa huo umekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha juhudi za Serikali katika masuala ya utunzaji na usimamizi wa mazingira kwa kuhimiza jamii umuhimu wa za uhifadhi wa mazingira ikiwemo upandaji miti na shughuli za usafi.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo










