Waziri Ndumbaro awasili mjini New York kushiriki Mkutano wa 50 wa Mwaka wa Uwindaji wa Kitalii

NA MWANDISHI MAALUM

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro amewasili mjini New York, Marekani leo tarehe 18 Januari 2022 kwa ajili ya kushiriki mkutano wa 50 wa mwaka wa Uwindaji wa Kitalii (Annual Hunting Convention) ulioandaliwa na Jumuiya ya Uwindaji ya Kimataifa.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro ( wa pili kulia) akiwa na ujumbe wake wakizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Elsie Kanza (katikati) mara baada ya kuwasili nchini Marekani kwa ajili ya kushiriki mkutano wa 50 wa mwaka wa Uwindaji wa Kitalii ( Annual Hunting Convention) ulioandaliwa na Jumuiya ya Uwindaji ya Kimataifa. 

Mkutano huo unaotarajiwa kuanza kesho tarehe 19 Januari, 2022 katika Jiji la Las Vegas, Nevada nchini Marekani umelenga kuwakutanisha watunga sera na wafanya maamuzi katika ngazi za juu kutoka nchi mbalimbali duniani kuweza kujadili masuala ya kisera katika kuendeleza sekta ya uwindaji.

Katika Mkutano huo, Dkt. Ndumbaro anatarajia kunadi fursa za uwekezaji za uwindaji wa kitalii zilizopo nchini Tanzania kwa lengo la kuwawezesha Matajiri wakubwa duniani kuchangamkia uwekezaji huo uliopo nchini Tanzania.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Marekani , Mhe. Elsie Kanza mara baada ya kuwasili nchini Marekani kwa ajili ya kushiriki mkutano wa 50 wa mwaka wa Uwindaji wa Kitalii ( Annual Hunting Convention) ulioandaliwa na Jumuiya ya Uwindaji ya Kimataifa.

Aidha katika mkutano huo Tanzania ni mshiriki muhimu ikizingatiwa kuwa Tanzania ni mojawapo ya nchi zinazoongoza duniani katika uhifadhi wa wanyamapori na uwindaji, Hivyo kupitia mkutano Tanzania itaweza kuongeza uelewa zaidi katika masuala ya kisera na maamuzi katika kuendeleza sekta ya uwindaji wa kitalii nchini.

Katika hatua nyingine, Dkt. Ndumbaro atapata fursa ya kufanya mazungumzo na Wadau mbalimbali wa masuala ya utalii waliopo nchini ikiwa ni nafasi adimu ya kuwavutia kuja kuwekeza nchini humo.
Kaimu Kamishna Uhifadhi wa TAWA, Mabula Misungwi akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Elsie Kanza mara baada ya kuwasili nchini Marekani kwa ajili ya kushiriki mkutano wa 50 wa mwaka wa Uwindaji wa Kitalii ( Annual Hunting Convention) ulioandaliwa na Jumuiya ya Uwindaji ya Kimataifa Katika mkutano huo, Waziri Ndumbaro ameambatana na Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Dkt. Maurus Msuha, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TAWA, Meja Jenerali, Hamis Semfuko, Kaimu Kamishna Uhifadhi wa TAWA, Mabula Misungwi, Wengine ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TAWA, Lulu Ng’wanakilala pamoja na Afisa Mhifadhi Mkuu wa Wanyamapori wa kutoka TAWA, Segolin Tarimo.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Elsie Kanza akisalimiana Afisa Mkuu wa Wanyamapori, Segolini Tarimo mara baada ya kuwasili nchini Marekani kwa ajili ya kushiriki mkutano wa 50 wa mwaka wa Uwindaji wa Kitalii (Annual Hunting Convention) ulioandaliwa na Jumuiya ya Uwindaji ya Kimataifa. 

Waziri Ndumbaro pamoja na ujumbe wake wamepokelewa na Mwenyeji wao  Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Elsie Kanza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news