WAZIRI UMMY ASHIRIKI MKUTANO WA 150 WA BODI TENDAJI YA WHO

NA MWANDISHI MAALUM

WAZIRI wa Afya, Mheshimiwa Ummy Mwalimu ameshiriki mkutano wa 150 wa Bodi Tendaji ya Shirika la Afya duniani ulioanza Januari 24 na utamalizika Januari 29,2022 kwa njia ya mtandao huku washiriki wengine wakiwa Wizara ya Afya kutoka Tanzania bara na Visiwani, Ofisi ya Rais TAMISEMI, pamoja na maafisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Uswisi.
Tanzania imewasilisha jumla ya maandiko 9 katika ajenda 8 za mkutano huu huku maeneo yaliyoandaliwa ni afya ya mama, mtoto na lishe, 

Magonjwa yasiyoambukiza, kifua kikuu, UKIMWI, magonjwa ya via vya uzazi na ngono, homa ya Ini, mafua makali ya influenza, polio na chanjo.

Waziri Ummy aliwasilisha andiko la afya ya kinywa na meno ambapo alitoa mwelekeo na mikakati ambayo Tanzania imejiwekea kuimarisha huduma katika eneo hilo.

Aidha, maandiko mengine yaliwasilishwa na wataalam mbalimbali waliohudhuria mkutano huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news