Waziri wa Fedha ateua wajumbe Bodi ya PSPTB

NA MWANDISHI DIRAMAKINI 

WAZIRI wa Fedha na Mipango,Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amefanya uteuzi wa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi nchini (PSPTB).

Uteuzi huo unakuja kufuatia uteuzi uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kumteua Bw. Jacob Kibona kuwa Mwenyekiti wa bodi hiyo hivi karibuni.
Wajumbe walioteuliwa na Mheshimiwa Waziri, Dkt.Mwingulu ni pamoja na Prof. O.A. Ndanshau,Bw. Evaristo Mwalongo,Bw. Ryagunga Mugetta,Bi. Esther L.J. Manyesha,Bw. Benezeth K. Ruta,Bw. Alban D. Mchopa,Bw. Oscar E. Mangula na Bw. Charles G. Mnyeti.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Benny Mwaipaja uteuzi wa wajumbe hao umeanza Desemba 19,2021.

Post a Comment

0 Comments