NA MWANDISHI MAALUM
"Gari la waandishi wetu wa Mkoa wa Mwanza lililokuwa kwenye ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza limepata ajali eneo la Busega lilikuwa linaelekea Ukerewe kwa kupitia Bunda.
"Nineongea na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, ndugu Gabriel (Mhandisi Robert Gabriel) amethibitisha kupokea taarifa za watu watano waliokuwa kwenye gari hilo lililobeba waandishi kufariki.Majina ya wenzetu hao tutayatoa kadri tutakavyofuatilia.
Kwa sasa Mkuu wa Mkoa nae anaelekea eneo la tukio nasi pia tunajipanga kwenda eneo la tukio.Naomba tuwe watulivu kwa wakati huu, wakati team yetu na ya Mkuu wa Mkoa tunafuatilia tukio hilo,"amefafanua Soko.