Ajali iliyochukua saa tisa Mlima Kitonga yasababisha taharuki

NA GODFREY NNKO, MLIMA KITONGA

ABIRIA wanaofanya safari zao kutoka miji mbalimbali kwa mabasi kutoka ndani na nje ya Tanzania yakiwemo magari binafsi wameshuhudia hadha kubwa ya usafiri kutokana na ajali iliyotokea katikati ya Mlima Kitonga mkoani Iringa.
Ajali hiyo ambayo imedumu kuanzia majira ya saa sita mchana hadi saa tano kasoro usiku wa Februari 13,2022 ilikata mawasiliano ya magari yote. Hivyo, hadi majira ya saa tano usiku wa Februari 13,2022 ndipo magari yameanza safari kuelekea Dar es Salaam, na Dar es Salaam kuelekea mikoa ya Nyanda za Juu Kusini,nchi jirani na kwingineko.
Ajali hiyo ilihusisha lori la mizigo ambalo
lililokuwa likirudi nyuma kwa dharura kwa kufeli breki, gari la Azam Media Limited (AML) na mengine.

Hivyo kusababisha taharuki kubwa, kwani licha ya moja wapo ya lori la mafuta kuwaka moto, wasamaria wema, zimamoto na wengine walijitolea kwa hali na mali kuudhibiti moto wa mafuta usienee kwa kasi, hali ambayo ingesababisha maafa makubwa kutokana na wingi wa magari  kutoka Iringa na yanayotokea Morogoro na watu.
Katika ajali hiyo ambayo DIRAMAKINI BLOG inasubiria taarifa rasmi kutoka Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa, imeshuhudia wafanyakazi zaidi 10 wa Azam Media Limited (AML) ambao walijeruhiwa huku gari lao likiharibika vibaya.

Aidha, Serikali ya Mkoa wa Iringa ilitoa msaada wa haraka kwa wafanyakazi hao ambao wamepelekwa kupatiwa matibabu.

Wafanyakazi hao walikuwa wanakwenda mkoani Mbeya kwa ajili ya kazi ya kurusha matangazo ya mechi za Ligi Kuu ya NBC.
Pia DIRAMAKINI BLOG imeshuhudia mamia ya wananchi wakigombania madumu ya mafuta ya kula katika ajali hiyo ambapo wengine walilazimika kutumia chupa za maji kuzijaza mafuta na kuondoka nayo wakati wengine wakiendelea na juhudi za uokoaji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news