Askofu Sothenes mgeni rasmi semina ya vijana Kanisa la Mtakatifu Bartolomeo

NA HUGHES DUGILO

ASKOFU wa Kanisa Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam, Jackson Sosthenes anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika semina maalum ya Umoja wa Vijana wa kanisa hilo ambapo pamoja na mambo mengine imelenga kuliombea Taifa.
Semina hiyo ambayo inatarajiwa kufanyika Februari 5, 2022 Katika Kanisa la Mtakatifu Bartolomeo lililopo Manispaa ya Ubungo mkoani Dar es Salaam pia makanisa yote ya Anglikana dayosisi hiyo yatahudhuria.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa umoja huo wa Vijana Dayosisi ya Dar es Salaam, John Kibata imesema lengo la kufanyika kwa semina hiyo ni kuliombea taifa, kanisa na kuwaleta pamoja vijana wote kwa ajili ya kufungua mwaka mpya.

Katika semina hiyo licha ya kuwa na matukio mbalimbali pia kutafanyika maombi maalum na semina maalum itakayoongozwa na Askofu wa Dayosisi hiyo,na matukio mengine mbalimbali.

Pia katika taarifa hiyo katika semina hiyo kwaya mbalimbali zitapata fursa ya kuimba nyimbo zao hivyo waumini wote wa kanisa hilo wametakiwa kujitokeza kwa wingi siku hiyo maalum.

Post a Comment

0 Comments