Rais Dkt.Mwinyi afanya uteuzi leo

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amemteua Ilyasa Pakacha Haji kuwa Mkurugenzi wa Mipango, Sera na Utafiti katika Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi.(Picha na Ikulu).

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Februari 2, 2022 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mhandisi Zena A. Said.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kabla ya uteuzi uliofanywa leo na Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi, Ilyasa alikuwa Afisa Mipango katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar.

Aidha, Mhandisi Zena A. Said kupitia taarifa hiyo ameeleza kuwa uteuzi huo wa Ilyasa umeanza leo Februari 2, 2022.

Post a Comment

0 Comments