Rais Dkt.Mwinyi afanya uteuzi leo

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amefanya uteuzi wa viongozi katika Wizara ya Maji, Nishati na Madini.
Hayo yamebainishwa kupitia taarifa iliyotolewa leo Februari 11, 2022 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mhandisi Zena A.Said.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua ndugu Maryam Issa Juma kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Sera na Utafiti.

Pia, Mheshimiwa Rais Dkt. Mwinyi amemteua ndugu Mwanamosi Ali Mwinchande kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Utumishi na Uendeshaji.

Aidha, taarifa hiyo iliyotolewa na Mhandisi Zena A.Said imefafanua kuwa, uteuzi wa viongozi hao umeanza leo Februari 11, 2022.

Post a Comment

0 Comments