Rais mstaafu Dkt.Kikwete: Rais Samia ameonesha maajabu makubwa katika kuiongoza Tanzania, tumuunge mkono

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

RAIS mstaafu wa Awamu ya Nne, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amesema Rais wa Awamu ya Sita, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameonesha maajabu makubwa katika kuiongoza nchi,hivyo wananchi wamuunge mkono.
Dkt.Kikwete ameyasema hayo Chalinze wilayani Bagamoyo wakati wa sherehe za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani kutimiza miaka 45.

Amesema, licha ya kuchukua madaraka katika kipindi kigumu kutokana na kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John Magufuli, Mheshimiwa Rais ameonesha ujasiri na kuonesha njia ya kuelekea kwenye mafanikio.

Aidha, amesema kuwa ameidhihirishia Tanzania na Dunia kuwa ana uwezo na jitihada za kuleta maendeleo kwa wananchi wake.
Akielezea juu ya uchaguzi wa ndani ya chama amewataka wana CCM kuchagua viongozi watakaotanguliza mbele maslahi ya chama siyo binafsi.

Amewataka kuwachagua viongozi ambao wataonesha njia kwani chama kina fedha na rasilimali.

Pia amewataka Watanzania kuendelea kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan ili maono ya kuiletea nchi maendeleo yaweze kufikiwa.

Dkt.Kikwete amesema,Rais Samia Suluhu Hassan ameonesha kujiamini jasiri, ujuzi, maarifa na uwezo na aliithibitishia Tanzania na dunia kuwa na uwezo wa kuongoza nchi inapiga hatua za maendeleo.

Amesema, ameweza kuiongoza nchi bila ya kutetereka baada ya kuchukua madaraka kufuatia kifo cha Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John Magufuli.

"Amefanya mambo makubwa na chama kimebaki vile vile na mambo mazuri yanakuja, kwani maono yake na mtazamo wake unaonesha njia, kwani hiyo ndiyo sifa ya kiongozi kwani ni kiongozi mchapa kazi hodari na jasiri, kikubwa tumuunge mkono,"amesema Dkt.Kikwete.
Aidha, kuhusu chama amesema kuwa angependa kuona chama kinajengwa na kuhamasisha kiwe na uhai kwa kulipa ada na kufanya mikutano na kuongeza wanachama na jumuiya za chama kazi yake ni kutafuta marafiki na kushiriki kazi za chama.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news