Siku ya Maadhimisho ya Redio Duniani 2022

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

KATIKA kuadhimisha Siku ya Redio Duniani 2022, ambayo kilele chake ni Februari 13 kila mwaka, Waandishi wa Habari, Mameneja wa Redio na Wahariri toka Redio mbalimbali mkoani Mwanza wamejumuika katika kongamano la pamoja lililofanyika mkoani hapa.
Akizungumza katika ufunguzi wa kongamano hilo, mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel, amesema Serikali inathamini nafasi ya Redio katika kusaidia maendeleo ya Mkoa na nchi ya Tanzania kwa ujumla.

Amesisitiza kuwa, wakati wowote ule Waandishi wa Habari za Redio wanayo fursa ya kukutana naye ofisini kwa ajili ya kuhabarisha na kuibua hoja za kimaendeleo mkoani Mwanza.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya Siku ya Habari kwa mwaka huu 2022 ni "Redio na Uaminifu" ambayo inasisitiza mambo makuu matatu; "Waandishi wa Redio kuwa wabunifu na waadilifu", "kuwajua wasikilizaji na kuwapatia maudhui yanayolingana na mahitaji" na "Redio kutengeneza vyanzo vya fedha ili kukabiliana na masuala ya kiuchumi".

Kongamano hilo limeratibiwa na Shirika la Internews, kwa kushirikiana na FHi360, na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza MPC ambayo iko chini ya Muungano wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news