STAMICO YAZIDI KUPAA, MGODI WA CHINI (UNDERGROUND MINE) KIWIRA UPO TAYARI KWA UZALISHAJI

NA MWANDISHI MAALUM

KAIMU Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Dkt. Venance Mwasse tarehe 29 Januari 2022 pamoja na viongozi wengine wa STAMICO wamepata fursa ya kujionea ukarabati mkubwa wa miundombinu ya mgodi wa chini (underground mine) katika Mgodi wa Kiwira kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa makaa ya mawe na kuhudumia wateja wengi zaidi (massive coal mining).
Katika ziara hiyo Dkt. Mwasse alipata maelezo na ufafanuzi wa ukarabati mbalimbali uliofanyika kutoka kwa mratibu wa mradi huo, Mhandisi Peter Maha ambaye alieleza mafanikio ya hatua mbalimbali zilizofanyika katika kukarabati mgodi huo ikiwa ni kurejesha njia za reli,mifumo ya hewa,maji na umeme.

Sambamba na matengenezo ya mikanda ya kusafirishia makaa kuja nje ya mgodi ambapo makadirio ya uzalishaji wa makaa kwa mwezi ni tani 5,000.

Aidha, hadi sasa ukarabati wa miundombinu wa mgodi umefikia asilimia 98 na kuwa tayari kwa uzalishaji.

Baada ya kutembelea mgodi huo wa chini Kaimu Mkurugenzi Mtendaji alipata fursa ya kuongea na wafanyakazi na kuwapongeza kwa kazi kubwa wanayofanya na hatua zilizofikiwa katika ukarabati wa mgodi huo. Vilevile aliwasisitiza kuendelea kufanya kazi kwa bidii na ubunifu ilikuweza kufikia malengo ya makusanyo yaliyowekwa kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Kwa upande wao watumishi wamemshukuru Kaimu Mkurugenzi Mtendaji kwa kuweza kuwatembelea na kuongea nao kuhusu mipango hiyo ya shirika. 

Aidha, wamemuahidi kuongeza juhudi katika kuchapa kazi ili malengo mbalimbali ya shirika waliyojiwekea yaweze kufikiwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news