Rais Samia amteua Zuhura Yunus kuwa Mkurugenzi mpya Mawasiliano ya Rais (Ikulu)

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amemteua aliyekuwa mtayarishaji wa vipindi na mtangazaji wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Bi. Zuhura Yunus kuwa Mkurugenzi mpya wa Mawasiliano ya Rais (Ikulu).

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu iliyotolewa leo Februari Mosi, 2022 na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais (Ikulu), Jaffar Haniu.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo Zuhura Yunus anachukua nafasi ya Jaffar Haniu ambaye atapangiwa majukumu mengine. “Uteuzi huo umeanza Januari 30, 2022”.

Zuhura ambaye amepata umaarufu kupitia kipindi cha Dira ya Dunia cha BBC hivi karibuni alitangaza mpango wake wa kuachana na shirika hilo na kuendelea na uandishi na mambo mengine nje ya BBC.

Aidha,taarifa ya Zuhura kuondoka BBC zilikuja miezi kadhaa baada ya kuandika kitabu chake cha wasifu wa Biubwa Amour Zahor mwanaharakati mwanamke wa kisiasa wakati wa mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964.

Kitabu hicho kinachohusu maisha na mchango wa mwanamama wa Kizanzibari Biubwa Amour Zahor katika Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12, 1964, pia kilizinduliwa Dar es Salaam, mnamo Novemba 13,2021, katika hafla iliyohudhuriwa na Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi pamoja na wanazuoni, waandishi wa vitabu, wanaharakati, waandishi wa habari na wananchi wengine.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news