Viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni leo Februari 28, 2022

NA GODFREY NNKO

PAUNDI ya Uingereza inanunuliwa kwa Shilingi 3060.94 huku ikiuzwa kwa Shilingi 3092.471 na Franka ya Burundi inanunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.21.
Aidha,dola ya Marekani nchini inanunuliwa kwa Shilingi 2286.823 huku ikiuzwa kwa Shilingi 2309.71.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Februari 28, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Wakati huo huo, Euro ya Ulaya inanunuliwa kwa shilingi 2563.321 na kuuzwa kwa shilingi 2589.416 na Yuan ya China inanunuliwa kwa shilingi 362.04 huku ikiuzwa kwa shilingi 365.6 na Yen ya Japan inanunuliwa kwa shilingi 19.80 na kuuzwa kwa shilingi 19.994.
Kwa upande wa Franka ya Rwanda inanunuliwa kwa shilingi 2.22 na kuuzwa kwa shilingi 2.29 huku shilingi ya Uganda ikinunuliwa kwa shilingi 0.62 na kuuzwa kwa shilingi 0.65.

Aidha, Randi ya Afrika Kusini inanunuliwa kwa shilingi 150.5 na kuuzwa kwa shilingi 151.91 huku shilingi ya Kenya ikinunuliwa kwa shilingi 20.10 na kuuzwa kwa shilingi 20.27.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news