Balozi wa Tanzania nchini Italia ateta na wadau wa NGOs zinazofanya kazi zake nchini Tanzania

NA MWANDISHI MAALUM

BALOZI wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo amekutana na kufanya mkutano na wadau wa NGO’s takribani 64 zinazofanya shughuli zake nchini Tanzania mwishoni mwa wiki jijini Roma, Italia.
Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mheshimiwa Mahmoud Thabit Kombo akipokea zawadi ya kitabu kutoka kwa mmoja wa wadau wa NGO’s mwishoni mwa wiki jijini Roma, Italia.

Mkutano huo ulihudhuriwa pia na wadau mbalimbali wa Diaspora pamoja na wadau wa NGOs walimpongeza Mhe. Balozi kwa kuwapa nafasi ya kujitambulisha na kutoa fursa ya kuwasikiliza mafanikio yao sambamba na changamoto wanazopitia katika kufanikisha shughulika zao nchini Tanzania.

Pamoja na kuwasikiliza, lakini pia Balozi alitumia nafasi hiyo kuwashauri kuwa na ushirikiano wa pamoja ili kuleta ufanisi zaidi kwenye maeneo wanayoyafanyia kazi.

Aidha, katika mkutano huo Balozi Kombo aliongea mubashara na Balozi wa Italia nchini Tanzania, Mhe. Marco Lombardi na kumpa fursa ya kutoa salaam zake moja kwa moja kwa njia ya mtandao.
Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akipokea akiwa katika kikao na wadau wa NGO’s mwishoni mwa wiki Jijini Roma, Italia.

Balozi wa Italia nchini Tanzania aliwahakikishia wadau hao kuwa wapo kwenye mikono salama ya Balozi wa Tanzania jijini Roma na chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Tanzania ni nchi salama ya kufanya shughuli zao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news