BALOZI WA MAREKANI APONGEZA UENDESHAJI MICHAKATO YA KISIASA NCHINI

NA MWANDISHI MAALUM

BALOZI wa Marekani nchini, Mhe. Dkt. Donald Wright amepongeza uendeshaji wa michakato ya kisiasa inavyoendeshwa nchini Tanzania.
Balozi wa Marekani nchini, Mhe. Dkt. Donald Wright akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Balozi Wright ameyasema hayo wakati alipokutana kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.

Balozi Wright amesema, anaridhishwa na jinsi hali ya kisiasa ilivyo hapa nchini na kuongeza kuwa anaunga mkono michakato ya kisiasa inavyoendeshwa nchini na kuelezea kuridhishwa kwake na hali hiyo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimueleza jambo Balozi wa Marekani nchini Mhe. Dkt. Donald Wright.
Kikao cha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Balozi wa Marekani nchini Mhe. Dkt. Donald Wright kikiendelea

Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Marekani kwa maslahi ya pande zote mbili.

Naye Waziri Mulamula amemuahidi Dkt. Wright kuwa Serikali itaendelea kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake wakati wote hapa nchini.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Balozi wa Norway nchini Mhe. Elisabeth Jacobsen katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akizungumza Afisa kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) Bibi. Jacqueline Machangu-Motcho katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Katika tukio jingine, Waziri Mulamula amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Norway nchini Mhe. Elisabeth Jacobsen na kujadili masuala ya ushirikiano katika masuala ya amani na usalama, jinsia na uwezeshaji wa wanawake.

Pia, Waziri Mulamula amekutana kwa mazungumzo na Afisa kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) Bibi. Jacqueline Machangu-Motcho na kujadili masuala ya ushirikiano baina ya mfuko huo na Tanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news