KADIO AAGIZA UONGOZI WA MFUKO WA FARAJA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI KUZINGATIA KATIBA NA MWONGOZO

NA MWANDISHI MAALUM-MoHA

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio ambaye pia ni Mlezi wa Mfuko wa Faraja ameagiza uongozi wa mfuko wa faraja wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuzingatia katiba na mwongozi wa mfuko huo kwenye ukusanyaji wa mapato, matumizi ya fedha za mfuko huo na huduma kwa wanachama wake.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Christopher Kadio ambaye pia ni Mlezi wa Mfuko wa Faraja akizindua Mfuko wa Faraja wa Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji jijini Dodoma.

Akizungumza na uongozi wa Mfuko wa Faraja wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi amewaelekeza kuingiza mchango wa mwajiri kwenye bajeti ya Wizara kwa Mwaka 2022/23 ili kuhudumua wanachama wa mfuko huo. Pia amewaagiza kufanya uchaguzi wa Uongozi wa kudumu wa mfuko ndani ya mwaka huu wa fedha.

"Mimi kama Mlezi wa Mfuko wa Faraja wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi nawasisitiza kuzingatia katiba na mwongozo wa Mfuko hii pamoja na kuingiza mchango wa nwajiri kwenye bajeti ya wizara," amesema.

Christopher Kadio alisema hayo leo Machi 11, 2022 kwenye uzinduzi wa Mfuko wa Faraja wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi uliofanyika katika ukumbu wa Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto, jijini Dodoma.

Aidha, amewashauri watendaji na watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kujiunga na Mfuko huo kwani faida zake ni nyingi na utawawezesha wafanyakazi kiuchumi na kuongeza tija kwenye majukumu yao.

Katibu Mkuu Christopher Kadio amesema kwamba Mfuko wa Faraja wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ni kama sehemu ya bima ya dharura na kwamba utasaidia kupunguza msongo wa mawazo wa changamoto za masuala ya dharura ya kijamii kama kuuguliwa na kufiwa.

“Licha ya kwamba kujiunga na Mfuko ni hairi ya mtu,lakini kwa faida nilizozieleza ni ushauri wangu kuwa watu wote wajiunge kwa kuzingatia faida nilizozieleza, Umojani nguvu na utengano ni udhaifu,"amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news