Mheshimiwa Kundo apita mtaa kwa mtaa kuhamasisha utekelezaji Mfumo wa Anuani za Makazi

NA MWANDISHI MAALUM

NAIBU Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Kundo Mathew (Mb) amewataka wakazi maeneo ya Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi kushiriki kikamilfu katika zoezi utekelezaji mfumo wa Anuani za Makazi pamoja na Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika mwezi Agosti, 2022.
Mheshimiwa Mhandisi Kundo ameyasema hayo Machi 10, 2022 wilayani ya Bariadi Mkoa wa Simiyu alipofanya ziara katika vijiji mbalimbali vya Wilayani humo ya kuhamasisha utekelezaji wa mfumo wa Anuani za Makazi naotakiwa kukamiliza ifikapo mwezi Mei 2022.

Alisema kuwa, wananchi wote wanaoshi katika Wilaya ya Bariadi wakashiriki kikamilifu katika utekelezaji mfumo wa Anwani za Makazi ili ukawe rahisi kwenda kutekeleza zoezi la Sensa ya watu na makazi litakalofanyika mwezi Agosti, 2022 ambalo litapelekea urahisi wa ufikishwaji wa huduma na maendeleo kwa wananchi wa maeneo hayo kuendana na idadi yao.

Nae Mkurugenzi wa Huduma za Posta wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Caroline Kanuti alitumia fursa hiyo kuwaelezea wakazi wa Bariadi umuhimu wa mfumo wa Anuani za makazi endapo watashiriki kikamilifu katika zoezi hilo.

“Pale ulipo unaweza ukapata tatizo, unauguliwa au nyumba imewaka moto au kuna mgonjwa anataka kupelekwa hospitali
unapiga simu unajitambulisha tu kwamba nipo kitongoji fulani unataja na namba ya nyumba yako kisha yule unaempigia simu atakuja mapka pale ulipo kwahiyo kupitia mfumo wa Anwani za makazi inakuwa rahisi kupata msaada,”amesema.

Alisema kuwa, mfumo wa Anwani za Makazi unarahisisha shughuli za mbalimbali ikiwemo za kilimo kwa kununua mazao au pembejeo za kilimo popote ulipo na bidhaa yako kukufikia kwa urahisi

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news