NA MWANDISHI MAALUM
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo,Mifugo na Maji imeitaka Serikali kuwekeza nguvu zaidi katika kutoa elimu kwa umma juu ya udhibiti wa sumukuvu ili kupunguza madhara yanayosababishwa na sumukuvu.
“Tunaipongeza Serikali kwa ujenzi wa maabara ya udhibiti wa magonjwa ya kibaolojia ya mimea,ambayo kukamilika kwake kutasaidia sana kupunguza matumizi ya kemikali kama viuatilifu katika mimea katika kudhibiti magonjwa na mashambulio ya wadudu waharibifu katika mimea.
"Aidha serikali ihakikishe inatoa elimu kwa umma na hasa kwa wakulima wadogo wadogo juu ya udhibiti wa sumukuvu katika mimea na kuelimisha wakulima juu ya matumizi ya wadudu marafiki katika kudhibiti magonjwa ya mimea,”amesema Dkt.Ishengoma.
Akitoa maelezo ya awali Naibu Waziri wa Kilimo,Mhe. Anthony Mavunde ameishukuru Kamati ya Bunge kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kusimamia na kuishauri serikali katika masuala yahusuyo kilimo na kuahidi kuyafanyika kazi maelekezo yaliyotolewa.
>Kujenga maghala 14 ya kuhifadhi mazao ya chakula;
>Ujenzi wa kituo mahiri cha usimamizi wa mazao baada ya kuvuna (Post harvest Center of Excellency)
>Ujenzi wa Maabara Kuu ya Kilimo.
0 Comments