KAMPUNI ZA KITANZANIA KUWEZESHWA KUPITIA PROGRAMU YA KUENDELEZA BIASHARA ZA WAZAWA INAYOTEKELEZWA NA MGODI WA DHAHABU WA NORTH MARA

NA MWANDISHI MAALUM

KAMPUNI ya madini ya Barrick Gold Corporation imetangaza kuwa kampuni 15 zimehitimu kutoka kwenye Progamu ya Kuendeleza Biashara za Ndani.
Wahitimu na wageni waliohudhuria hafla hiyo wakifuatilia matukio.

Tangu kuanzishwa kwa programu hiyo mwezi Novemba mwaka 2021, kampuni za ndani ya nchi zimepatiwa mafunzo mara nne kwa nyakati tofauti katika kipindi cha miezi minne kwa lengo la kujenga uwezo na kusaidia ziweze kunufaika na fursa zilizopo kwenye sekta ya madini.
Wahitimu wakiwa katika picha ya pamoja.

Programu hii imefadhiliwa na Kampuni ya Barrick na imetekelezwa na kampuni ya Kengo kwa kushirikiana na Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) na imekuwa ikitoa mafunzo ya kitaalam na ushauri wa kibiashara kwa makampuni madogo na ya kati ili kuziimarisha kiujuzi na kuziwezesha kunufaika na mnyororo wa thamani wa sekta ya madini.

Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Barrick, Mark Bristow amesema kuwa programu hiyo ni ya kwanza na kipekee kwenye sekta ya madini na amewasihi wengine kufuata mfano huo.

“Tunajivunia kwa kuongoza njia kwa kufanikiwa kuendesha program hii ya maendeleo ya biashara za ndani ya nchi na tumetimiza wajibu zaidi ya sheria zilizopo maudhui ya ndani. Maudhui ya ndani ni muhimu kwa shughuli zetu na tunapoziimarisha kampuni ndogo na za kati, tunaziimarisha na jamii zinazotuzunguka. Barrick itaendelea kuunga mkono maendeleo ya kampuni ndogo na za kati ambazo ni muhimu sana katika ukuaji wa uchumi,” alisema.
Kamishna wa Tume ya Madini, Janeth Reuben akiwahutubia wahitimu na wageni waalikwa wakati wa mahafali hayo.

Programu hii imeshuhudia mafanikio makubwa kama vile utengenezaji wa mipango mikakati kwa ajili ya makampuni yanayoshiriki, kuimarishwa kwa mzunguko wa fedha na uunganishwaji wa fursa mbalimbali za kibiashara.

Wahitimu pia wameweza kunufaika na mafunzo kutoka Wizara ya Madini, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), washauri wa rasilimali watu, na taasisi za kifedha.
Kamishna wa Tume ya Madini, Janeth Reuben akikabidhi cheti kwa Mwenyekiti wa Kikundi cha vijana cha Wings Yusuph Gesase wakati wa mahafali hayo.
Mmoja wa wahitimu Judith Mweta, kutoka kampuni ya Gree Culture TZ Ltd, akipokea cheti kutoka kwa Kamishna wa Tume ya Madini, Janeth Reuben (Kulia)
Mkuu wa wilaya ya Tarime Kanali Michael Mtenjele, akiongea na wahitimu na wageni waalikwa wakati wa mahafali hiyo.

Shack Noels kutoka kampuni ya EHS Company Limited amesema kuwa programu hiyo imeitambulisha biashara yake kwenye viwango vya kimataifa vya utendaji jambo linalomlazimu kuboresha ubora wa huduma zake za ukandarasi.

Kupitia mafunzo baina ya mkufunzi na mshiriki, makampuni hayo yameweza kuungana na mtandao wa ikolojia ya uchimbaji madini na kutambua maeneo ya ukuaji.
Meneja wa Mahusiano wa Kijamii wa Barrick North Mara Gilbert Mworia, akiongea na wahitimu na wageni waalikwa wakati wa mahafali hiyo.
Baadhi ya wahitimu wakibadilishana mawazo wakati wa hafla hiyo.

Janeth Reuben Lekashingo, Kamishna wa Kamisheni ya Madini amesema: Serikali kupitia Kanuni ya Kushirikisha Wananchi katika Mnyororo wa Uchumi wa Madini ya Mwaka 2017 imetoa mfumo wezeshi kwa ajili ya biashara za ndani ili zinufaike kutoka kwenye uwekezaji unaofanywa nchini kupitia fursa zilizopo kwenye mnyororo wa thamani.

Aidha, Program ya Kuendeleza biashara za ndani wa Mgodi wa Dhahabu North Mara umeweka viwango ambavyo makampuni mengine yanaweza kufuata.

Halfa ya mahafali hayo ilihusisha wageni waalikwa wakiwemo wakufunzi, Maafisa wa Serikali, Taasisi za Kifedha na Wabia katika Sekta ya Madini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news