Augustino Lyatonga Mrema kuoa wiki ijayo, asema amepata binti mdogo mrembo

NA MWANDISHI MAALUM

MWENYEKITI wa TLP Taifa, Augustino Lyatonga Mrema ametangaza kufunga ndoa siku ya Machi 24, 2022 katika Parokia ya Uwomboni kijijini kwake Kiraracha mkoani Kilimanjaro.

Mrema mwenye umri wa miaka 77 ambaye pia ni Mwenyekiti wa bodi ya Parole Nchini anafunga ndoa hiyo mara baada ya kumpoteza mke wake Rose Mrema aliyefariki dunia mwaka jana.

Mrema amesema amepata, binti mwenye umri mdogo mweupe ambaye ni chaguo lake na watafunga pingu za maisha baada ya kufuata taratibu zote za kikanisa pamoja na ulipaji wa mahari.

Amesema,kilichomsukuma kuoa ni kumpata msaidizi wa maisha yake kwani yeye ni mzee na anahitaji mtu wa karibu wa kumwangalia na kumsaidia kwa ukaribu huku akiishukuru familia yake kwa kumkubalia.

Post a Comment

0 Comments