Mabinti wa Kitanzania watembeza kichapo cha mabao 7-0 kwa Botswana

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

TIMU ya Taifa ya wasichana chini ya umri wa miaka 17 (U17) imeitandika Botswana mabao 7-0.

Ni kupitia mtanange uliopigwa katika dimba la Amaan jijini Zamzibar ikiwa ni mchezo wa Raundi ya Pili kufuzu Kombe la Dunia baadaye mwaka huu nchini India.
Neema Paul na Clara Luvanga kila mmoja alifunga mabao mawili na Aisha Juma alifunga mabao matatu.

Aidha, timu hizo zitarudiana Machi 20, mwaka huu katika dimba la Obed Itani Chilume katika Jiji la Francistown ambalo ni la pili kwa ukubwa nchini Botswana.

Katika mtanange huo, mshindi wa jumla atakutana na Burundi katika Raundi ya Tatu kuwania kwenda Raundi ya mwisho ya mchujo kulingana na ratiba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news