Machi 19, 2022 ni Mjadala wa Kitaifa katika Sekta ya Sanaa na Michezo mbalimbali kuelekea Mwaka Mmoja wa Rais Samia madarakani USIKOSE!

WATCH Tanzania inakualika kushiriki Mkutano utakaofanyika Machi 19, 2022 (Jumamosi) kupitia Mtandao wa Zoom kuanzia saa 10 kamili jioni hadi 12:30 jioni.
Mkutano huu utajadili;Maendeleo katika Sekta ya Sanaa na Michezo mbalimbali kuelekea Mwaka Mmoja wa Rais Samia Madarakani

Muda ukifika (Saa 10 kamili, Machi 19, 2022 - Jumamosi) utaweza kujiunga na kushiriki moja kwa moja kwa kubofya hapa https://bit.ly/34HGZhk

Au kupitia

Meeting ID: 89308078223

Passcode: 786246

Mkutano huu utarushwa mubashara (Youtube) kupitia EATV, Millard Ayo, Clouds Digital, Global TV Online, Dar Mpya TV, Sauti Kuu, TBC Online, Mwanahalisi Digital, Mwananchi Digital, EFM Digital, Star TV, Saangapi TV, Daily News Digital, ITV na Azam TV.

Karibu tujadili kwa pamoja maendeleo katika Sekta ya Sanaa na Michezo mbalimbali kuelekea Mwaka mmoja wa Rais Samia Madarakani. Usikose.

Mkutano huu umedhaminiwa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania - TADB na Mtandao wa Simu wa Airtel - Tanzania

Post a Comment

0 Comments