Makamu wa Rais ashiriki ufunguzi Jukwaa la Nane la Wakuu wa Nchi na Serikali Duniani huko UAE

NA MWANDISHI MAALUM

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.Philip Mpango leo Machi 29,2022 ameshiriki ufunguzi wa Jukwaa la 8 la Wakuu wa Nchi na Serikali Duniani linalofanyika Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu.
Makamu wa Rais anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika jukwaa hilo ambapo

Pamoja na mambo mengine lina lengo la kuimarisha ushirikiano wa kimataifa na kubadilishana mbinu za kuimarisha utendaji wa serikali.

Katika Ufunguzi wa Jukwaa hilo viongozi wakuu wa serikali, mashirika ya kimataifa pamoja na sekta binafsi kutoka nchi mbalimbali wamekutana na kujadili namna bora ya kuongeza ufanisi katika utoaji huduma za serikali kwa wananchi na kutatua changamoto mbalimbali kupitia utafiti kwa kuzingatia mabadiliko yanayoendelea duniani.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango leo tarehe 29 Machi 2022 akishiriki ufunguzi wa Jukwaa la 8 la Wakuu wa Nchi na Serikali Duniani linalofanyika Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu.

Hapo kesho tarehe 30 Machi 2022 Makamu wa Rais Dkt. Mpango anatarajiwa kuzungumza katika jukwaa hilo akichangia mada ya “Kwa nini Afrika imekua ni muhimu sana kwa wakati huu katika uchumi wa Dunia”.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news