Mambo ya Ndani yarekodi mafanikio makubwa, Waziri Masauni asisitiza

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

SERIKALI ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan imewezesha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupiga hatua kubwa ndani ya mwaka mmoja madarakani.
Miongoni mwa mafanikio hayo ni pamoja na kuimarika kwa hali ya ulinzi na usalama, kupandishwa vyeo kwa maafisa, wakaguzi na askari,kukamilisha malipo ya stahiki za Maafisa, wakaguzi, wskari na watumishi raia.

Pia kutoa ajira kwa askari wapya kukamilisha malipo ya wazabuni na watoa huduma mbalimbali ikiwemo kutoa mafunzo kwa maafisa, wakaguzi na askari kwa ajili ya upandishwaji vyeo.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ameyasema hayo Machi 14, 2022 jijini Dar es Salaam wakati akizungumzia mafanikio ya wizara yake katika mwaka mmoja wa uongozi wa Rais Samia madarakani.

Mhandisi Masauni ameyataja mafanikio mengine kuwa ni ujenzi wa ofisi, vituo vya polisi na nyumba za makazi kwa maafisa na askari wa vyombo vya ulinzi na usalama vilivyo po chini ya wizara hiyo, kutoa nishani, kwa viongozi,maafisa navyombo vya usalama.

“Miradi iliyotekelezwa ni pamoja na Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, Idara ya Uhamiaji, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, makusanyo ya maduhuli,ajira kwa askari, mabadiliko ya sheria mbalimbali, usajili na utambuzi wa wananchi, kupambana na biashara haramu ya usafirishiji wa binadamu.

"Kupunguza msongamano wa wafungwa, kupunguza gharama na urekebishaji wa wafungwa, masuala ya huduma kwa wakimbizi na kuimarishwa kwa ushirikiano wa kimataifa na kikanda katika kuzuia na kutanzua uhalifu nchini,”amefafanua Waziri Mhandisi Masauni.

Mbali na hayo Waziri Masauni amesema, maafisa wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali walipata mafunzo ambayo yamewaongezea uwezo wa kiutendaji na kuleta ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao.

“Jumla ya Maafisa Wakaguzi na Askari 34,000 wamehudhuria mafunzo ya kada mbalimbali kulingana na nafasi zao ambapo Jeshi la Polisi, Maafisa Wakaguzi na Askari 24,285 wamehudhuria mafunzo husika, Jeshi la Magereza, Maafisa Wakaguzi na Askari wamehudhuria mafunzo husika, 8,181, Idara ya Uhamiaji, Maafisa Wakaguzi na Askari wamehudhuria mafunzo husika ambapo Maafisa 336 na Askari 344 jumla yao ni 780 na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Maafisa Wakaguzi na Askari wamehudhuria mafunzo husika 918,”amesema.

Aidha Waziri Masauni alisema Katika kipindi cha mwaka mmoja wa Mhe. Samia Suluhu Hassan, jumla ya Maafisa, Wakaguzi, Askari na Watumishi raia 34,698 wamepandishwa vyeo, ambapo kati yao; 34,106 ni Maafisa, Wakaguzi na Askari na 592 ni Watumishi raia ambao walistahili kupandishwa vyeo katika kipindi cha mwaka wa fedha 2018/2019, 2019/2020 na 2020/2021

Kuhusu NIDA Masauni alisema Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imefanikiwa kusajili wananchi 1,061,998 katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita, hivyo kufanya jumla ya Wananchi 22,881,902 tangu kuanzishwa kwa Mamlaka hiyo.

Mbali na hayo Waziri Masauni alisema Wizara kupitia Sekretarieti ya Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu imefanikiwa kutoa mafunzo kwa wadau 280 wanaohusika na utekelezaji wa Sheria ya Kuzuia Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu.

Waziri Masauni alimaliza kwa kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo ameiwezesha wizara hiyo na taasisi zake zote ikiwemo Vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyopo chini ya wizara hii, kupata mafanikio makubwa tangu alipoingia madarakani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news