Mihambwe wajivunia mwaka mmoja wa Rais Samia madarakani

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

AFISA Tarafa wa Mihambwe mkoani Mtwara, Emmanuel Shilatu amezungumzia mwaka mmoja wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan madarakani kuwa wenye mafanikio na wakijivunia mafanikio tele yaliyopatikana kwenye nyanja mbalimbali za kielimu, afya, kichumi na kijamii.
Hayo yamejiri kwenye kikao kazi alichokifanya Gavana Shilatu kuzungumza na viongozi ambapo amekiri Rais Samia kufanya mambo makubwa ndani ya mwaka mmoja wake madarakani.

"Kwa niaba ya wananchi Tarafa ya Mihambwe tunajivunia mwaka mmoja wa Rais Samia madarakani umejaa amani, utulivu, maendeleo na neema tele kwa Tarafa ya Mihambwe. 
 
"Mathalani Rais Samia ameleta shilingi 500,000,000 kujenga kituo cha afya cha Tarafa ya Mihambwe, Rais Samia ameleta shilingi 420,000,000 kujenga madarasa 21 shule za sekondari na msingi.
"Rais Samia ameleta fedha kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo, fedha kwa ajili ya kutoa huduma kwa jamii, Rais Samia ameendelea kuleta fedha kutoa elimu bure. Kiukweli Rais Samia ameupiga mwingi sana kwetu wana Tarafa ya Mihambwe na viunga vyake. Asante sana Rais Samia kwa kutupenda Watanzania,"amesema Gavana Shilatu.

Gavana Shilatu pia aliwasisitiza viongozi kuwa wadau wazuri kueleza mambo mazuri yaliyofanywa na Rais Samia kwa wananchi kupitia mifano halisia ya kimaendeleo iliyopo kwenye maeneo yao.
Wakati huo huo, Gavana Shilatu amefanya ziara kutembelea miradi mbalimbali ya kimaendeleo ambapo amesisitiza uwazi, ushirikishwaji, ufanisi, kasi kuikamilisha kwa wakati na ubora unaolingana na thamani ya fedha.
Katika ziara hiyo Gavana Shilatu aliambatana na viongozi Serikali ya Kijiji, viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliokuwa wakikagua utekelezaji ilani ya uchaguzi CCM ambapo wameridhishwa na utekelezaji wake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news