Msemaji wa Simba SC amtembelea Sheikh Mkuu wa Tanzania nyumbani kwake

>Mufti afurahia mwaliko wa Aprili 3,mwaka huu uwanja wa Benjamin Mkapa

NA MWANDISHI MAALUM

MENEJA wa Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Ahmed Ally hii leo amemtembelea nyumbani kwake Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Abubakar Bin Zubeiry bin Ally.
Katika ziara hiyo, Ahmed amemkabidhi Mufti zawadi ya jezi na kumpa mwaliko wa kuhudhuria mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya US Gendemarie utakaopigwa Aprili 3, mwaka huu katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Akipokea zawadi hiyo Mufti ameeleza kufurahishwa na ziara ya Meneja wa Simba na kueleza kuwa ameonesha heshima ya kuwathamini wakubwa.
Kuhusu mwaliko wa kwenda uwanjani Mufti amesema, amefurahi sana kwani ana muda mrefu hajaenda uwanjani na kama haitoshi mpira wa miguu unaondoa msongo wa mawazo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news