Mtanzania azimegea kampuni, taasisi mbinu za kuyapa kisogo mashambulizi ya mitandaoni

NA GODFREY NNKO

MTANZANIA ambaye ni Mtaalam na Mbobezi wa Usalama Mtandao na Uchunguzi wa Makosa ya Kidigitali, Yusuph Kileo ameendelea kutoa wito kwa taasisi na kampuni mbalimbali nchini kuwekeza zaidi kwenye udhibiti wa uhalifu mtandao ili kuepuka mashambulizi ambayo yamekuwa yakigharimu rasilimali fedha nyingi.
Kileo ametoa rai hiyo baada ya DIRAMAKINI BLOG kutaka kufahamu ni upi wito wake kwa taasisi hizo ikiwa ni siku chache zimepita baada ya Kampuni ya Toyota kutangaza itasitisha kuendelea na shughuli zake kufuatia shambulizi la mtandaoni.

Amesema, udhibiti wa uhalifu mtandao unaweza kupunguza tatizo kwa kiasi kikubwa na kwa gharama nafuu kulinganisha na kushughulikia tatizo linapokuwa kimetokea.
"Tumekuwa na mashambulizi kadhaa yanayoendelea hususani yanayojihusisha na 'supply chain' (ugavi). Tumeendelea kutoa wito wa makampuni kufunga mikanda kudhibiti uhalifu mtandao ili kujiweka mbali na kukabiliana na athari kubwa za uhalifu mtandao unaotegemewa kukua kwa kasi siku za usoni,"amesema Bw.Kileo

Pia amesema, huu ni wakati wa kutumia elimu ya uelewa kutoka kwa watu sahihi wenye uelewa na uwezo wa kudhibiti uhalifu mtandao.

"Kuwaongezea uwezo watu hao sahihi ni njia za awali zinazopaswa kufanyiwa kazi na makampuni yetu. Aidha, kuimarisha ushirikiano wa ndani na kwa mataifa mengine ikiwemo kutumia tools sahihi na madhubuti za udhibiti ni mambo muhimu pia ya kuzingatia,"amefafanua Bw.Kileo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news