Ndugu zangu, itunzeni hii barabara-Ndejembi

NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amewataka wananchi wa Kijiji cha Nange wilayani Misungwi kuhakikisha wanaitunza barabara ya jamii yenye urefu wa kilometa 2.6 inayojengwa na TASAF kupitia mradi wa utoaji ajira za muda kwa walengwa, ulioibuliwa na wananchi wa eneo hilo kutokana na uhitaji wa barabara itakayowawezesha kusafiri ili kupata huduma muhimu za kijamii.
"Barabara hii inajengwa kwa fedha za Serikali kupitia TASAF, tukiendelea kuacha ng’ombe wapite na mvua ikinyesha tu itageuka kuwa tope na kuwapa changamoto ya kutokuwa na barabara itakayowawezesha kupata huduma za kijamii kama afya, elimu na usafiri,” Mhe. Ndejembi amesisitiza.

Post a Comment

0 Comments