Rais Samia awaapisha Balozi Polepole, RC Waziri Kindamba


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Humphrey Polepole kuwa Balozi wa Tanzania katika nchi ya Jamhuri ya Malawi kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma leo Machi 15, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Waziri Kindamba Waziri kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Malawi Humphrey Polepole mara baada ya hafla fupi ya Uapisho iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Waziri Kindamba mara baada ya hafla fupi ya Uapisho iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassoro Mbarouk, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Kattanga katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Waziri Kindamba Waziri na Balozi wa Tanzania nchini Malawi Humphrey Polepole mara baada ya tukio la Uapisho Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali mara baada ya hafla ya Uapisho iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma leo Machi 15, 2022. (Picha na Ikulu).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news