RC Kitwana: Ushirikiano baina ya Jeshi la Polisi, waandishi wa habari ni jambo la heri sana

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

MKUU wa Mkoa Mjini Magharibi, Mheshimiwa Idirisa Kitwana Mustafa amewataka waandishi wa habari nchini kushirikiana na Jeshi la Polisi katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuona taaluma hiyo inaendelea kubakia salama.
Mheshimiwa Kitwana amesema hayo alipokuwa akifungua mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali na Jeshi la Polisi yanayohusiana na usalama kwa waandishi wa habari na jeshi hilo Mkoa wa Mjini Magharibi.

Mafunzo ambayo yalifanyika katika ukumbi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) uliopo Wilaya ya Mjini Unguja.

Amesema, waandishi wa habari na Jeshi la Polisi ni vyombo vinavyofanya kazi kwa pamoja hivyo ni vyema wakawa na ushirikiano wa karibu ili kufanikisha utendaji wa majukumu yao ya kila siku.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news