Serikali kuimarisha mikakati ya kukabiliana na maafa nchini

>Waziri Balozi Dkt.Chana aieleza Kamati ya Bunge hatua zinazoendelea kutekelezwa ikiwemo shuleni, vyuoni

NA MWANDISHI MAALUM

SERIKALI imesema inaendelea kuweka mikakati madhubuti juu ya namna ya kujikinga na kukabiliana na maafa ili kuepuka madhara makubwa yanayoweza kujitokeza na kuhatarisha usalama wa raia pamoja na kuharibu miundombinu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. Balozi. Dkt.Pindi Chana akizungumza wakati wa semina kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu dhana na Mfumo wa Usimamizi wa Maafa nchini iliyofanyika Machi 12, 2022 katika Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma. (Picha zote na OWM).

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. Balozi Dkt.Pindi Chana katika semina kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu dhana na Mfumo wa Usimamizi wa Maafa nchini iliyoandaliwa na Idara ya Menejimenti ya Maafa katika Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakichangia hoja katika semina hiyo kuhusu dhana na Mfumo wa Usimamizi wa Maafa nchini iliyofanyika Machi 12, 2022 katika Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Dkt.Joseph Mhagama akieleza jambo wakati wa semina kwa kamati hiyo kuhusu dhana na Mfumo wa Usimamizi wa Maafa nchini iliyofanyika Machi 12, 2022 katika Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.

“Hivi sasa Mheshimiwa Mwenyekiti nikuhakikishie elimu inayotolewa katika shule zetu za Msingi Sekondari na ngazi ya vyuo vikuu inalenga vijana wetu na jamii yetu kujua maafa kwa ujumla ili kujikinga wasipate madhara,”amesema Mhe.Pindi.

Aidha, alibainisha kwamba utafiti unaofanywa na watalaamu mbalimbali kuhusu Mazingira na Maafa utumike vyema kama moja ya njia ya kukabili maafa ya asili na yale yatokanayo na shughuli za kibinadamu. Utafiti hutoa mwanya wa kujua hatua sahihi za kuchukua kabla ya majanga kutokea na baada ya kutokea.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Bw. Kaspar Mmuya akifafanua jambo wakati wa semina kwa Kamati hiyo kuhusu dhana na Mfumo wa Usimamizi wa Maafa nchini iliyofanyika Machi 12, 2022 katika Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.

Wakati huo huo Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Bw. Kaspar Mmuya alifafanua kwamba Muswada wa Sheria ya Maafa utasaidia kuondoa changamoto zilizobainika kutokana na sheria ya zamani na wahusika kufahamu majukumu yao ili kuepusha muingiliano wa majukumu wakati wa utekelezaji wa shughuli zote za maafa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. Balozi Dkt.Pindi Chana akizungumza wakati wa semina kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu dhana na Mfumo wa Usimamizi wa Maafa nchini iliyofanyika Machi 12, 2022 katika Ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Mhe. Najma Giga alishauri Mfuko wa Maafa kutengewa bajeti yake itakayosaidia kutatua changamoto zinazotokana na Maafa badala ya kusubiri hadi yatokee na kuanza kutafuta wadau kwa ajili ya kutoa huduma.

“Tunaelewa waziwazi kuna Maafa ya kimaumbile ambayo huwenda yakatokea kila mwaka kutokana na mvua za masika au mabadiliko ya tabianchi kwenye fukwe zetu za bahari tunajua kabisa kila mwaka mabadiliko ya tabia nchi yanapotokea shemu ya ardhi inaliwa lakini ikitokea Maafa ndio tunaanza kupambana kutafuta wadau. Mfuko unaanza kutuna kwanini sasa serikali isione utaratibu utakaowekwa maalumu kwa hao hao watu wanaotusaidia,”alieleza Makamu Mwenyekiti huyo.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu,Bw.Charles Msangi akiwasilisha Dhana na Mfumo wa Usimamizi wa Maafa Nchini katika semina kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria iliyofanyika Machi 12, 2022 katika Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.

Akihitimisha wasilisho la dhana na Mfumo wa Usimamizi wa Maafa katika semina hiyo Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Bw. Charles Msangi alisema Muswada wa Sheria imezingatia uwajibikaji wa wadau wote kwani ulifanyika utafiti ambao uliangalia majukumu ya kila muda.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news