Serikali yatoa ombi maalumu kwa viongozi wa dini kuhusu Sensa, malezi ya kiroho

>Waziri Dkt.Mabula amwakilisha Waziri Mkuu katika ufunguzi wa Kanisa jipya la Bikira Maria wa Fatima Geita

NA MUNIR SHEMWETA-WANMM

SERIKALI imewataka viongozi wa dini nchini kuwaelimisha waumini wake umuhimu wa kuhesabiwa katka Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika mwezi Agosti, mwaka huu.
Askofu wa Jimbo Katoliki la Geita, Mhashamu Flavian Kassala akikata utepe wa ufunguzi wa Kanisa jipya la Bikira Maria wa Fatima. Wa pili kulia ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula ambaye alikuwa mgeni rasmi akimwakilisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Askofu wa Jimbo Katoliki la Geita, Mhashamu Flavian Kassala akifungua rasmi lango Kuu la Kanisa jipya la Bikira Maria wa Fatima Geita katika hafla ya Kutabaruku kanisa hilo iliyofanyika Machi 20,2022.

Aidha, imewataka viongozi wa dini kuendelea kusaidia katika suala zima la malezi ya kiroho ili kujenga jamii yenye kumcha Mungu, uadilifu na ubinadamu.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati wa Kutabaruku Kanisa la Bikira Maria wa Fatima Geita tarehe 20,2022, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula amesema, Tanzania imebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi ambazo bila ya kuwa na takwimu sahihi haitaweza kupanga mipango thabiti ya matumizi endelevu ya rasilimali hizo.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula akimpatia zawadi Askofu wa Jimbo Katoliki la Geita, Mhashamu Flavian Kassala wakati wa hafla ya kutabaruku Kanisa jipya la Bikira Maria wa Fatima Geita.

‘’Viongozi wa dini mnao waumini wengi tumieni fursa hiyo kuwaelimisha waumini wenu umuhimu wa kuhesabiwa,’’ ilieleza hotuba ya Waziri Mkuu.

Alisema, zoezi la sensa ya watu na makazi ni muhimu kwa kuwa linaipatia nchi takwimu za msingi zinazotumika kutunga sera, kupanga mipango na program za maendeleo pamoja na kufuatilia utekelezaji wake.

Kupitia hotuba hiyo, Dkt.Mabula alieleza kuwa, takwimu rasmi zitawezesha serikali na wadau wengine kufuatilia na kutathmini malengo yaliyofikiwa katika kutekeleza mipango ya maendeleo iliyokusudiwa sambamba na changamoto mbalimbali zitakazojitokeza katika sekta zote na hatimaye kuweka malengo na mikakati ya kukuza uchumi pamoja na kupunguza umasikini miongoni mwa watanzania.
Askofu wa Jimbo Katoliki la Geita Mhasham Flavian Kassala akipaka moja ya nguzo 12 za Kanisa mafuta ya krisma ndani ya kanisa mbele ya waumini wakati wa hafla ya kutabaruku Knisa jipya la Bikira Maria wa Fatima Geita.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akikabidhi cheti kwa baadhi waumini wakati wa hafla ya kutabaruku Kanisa jipya la Bikira Maria wa Fatima Geita.

Aidha, ilieleza kuwa, hivi karibuni kumekuwa matukio yanayohusisha mauaji ya raia kwa raia , moto kwenye masoko na baadhi ya raia kujinyonga ambapo alisema tayari serikali imeanza kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kulitaka jeshi la polisi kuweka mikakati ya kuhakikisha jamii inatoa taarifa sahihi zitakazosaidia kukabiliana na vitendo vya kihalifu.

‘’Niwaombe viongozi wetu wa taasisi za dini kuendelea kusaidia katika suala zima la malezi ya kiroho ili kujenga jamii yenye kumcha Mungu, uadilifu na ubinadamu," ilieleza hotuba ya Waziri Mkuu.

Kwa upande wake Askofu wa Jimbo Katoliki Geita, Mhashamu Baba Askofu Flavian Kasala ambaye ni Padre wa kwanza wa Parokia hiyo ya Bikira Maria wa Fatima tangu kuanzishwa kwake alisema, viongozi wa dni wataendelea kuiunga mkono serikali katika suala zima la sensa ya watu na makazi kwa kuwa suala hilo ni muhimu kwa maendeleo ya nchi.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya waumini waliochangia Samani za Kanisa jipya la Bikira Maria wa Fatima Geita kwenye hafla maalum ya Kutabaruku kanisa hilo ambapo alimuwakilisha Waziri Mkuu.

‘’Sisi tutaendelea kuinga mkono serikali na uwepo tofauti ndogo ndogo ndizo zimewapeleka baadhi ya watu kwenye matatizo makubwa na tusiruhusu jambo hilo linaloweza kututofautisha kwenye imani zetu za kidini,’’alisema Askofu Flavian Kasala.

Hafla ya kubariki Kanisa la Bikira Maria wa Fatima Jimbo la Geita ambalo ujenzi wake ulianza Januari 3, 2020 na kukamilika Machi 18, 2022 na kugharimu takribani shilingi Bilioni 1.9 iligawanyika sehemu ya kutabaruku kanisa kwa kunyunyizia maji ya Baraka nje na ndani ya kanisa, kupaka mafuta ya krisma altare mpya pamoja na nguzo 12 na kuendelea na ibada ya misa takatifu iliyoanza saa tatu asubuhi hadi saa kumi jioni.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt.Angeline Mabula akiwahutubia waumini waliohudhuria hafla ya Kutabaruku Kanisa la Bikira Maria wa Fatima Geita iliyofanyika Machi 20,2022 ambapo alimuwakilisha Waziri Mkuu.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula akiwa katikati ya Mapadre wakati wa kuendesha harambee ya kuchangia samani za kanisa jipya la Bikira Maria wa Fatima Geita katika hafla maalum ya Kutabaruku kanisa hilo ambapo alimuwakilisha Waziri Mkuu.

Aidha, kupitia hafla hiyo Dkt.Angeline Mabula aliongoza harambee kwa ajili ya kuchangia ukamilishaji samani za kanisa ambapo kiasi cha shilingi 88,725,000 kilipatikana kwa fedha taslimu na ahadi kutoka kwa watu mbalimbali.

‘’Uwepo wa jengo hili jipya, kubwa na zuri la Kanisa la Bikira Maria wa Fatima ni ushuhuda wa kukua kwa imani ya kanisa kwa waumini wake ambapo sasa ni miaka 65 imepita tangu injili ilipoingia ukanda huu wa Altare ya kwanza ya Jimbo la Geita ilikuwa katika uwanja lililopojengwa jengo hili jipya,’’ alisema Askofu Kasala.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news