Ujenzi wa Maabara Changamana Awamu ya Pili mbioni kukamilika, Kamati ya Bunge yaipongeza TAEC kwa kazi nzuri

NA MWANDISHI MAALUM

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii imeipongeza Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) kwa hatua iliyofikia katika utekelezaji wa Ujenzi wa Maabara Changamana Awamu ya Pili.
Kamati hiyo Machi 15, 2022 ilifanya ziara Makao Makuu ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) ili kukagua maendeleo ya mradi huo wa ujenzi wa Maabara Changamana Awamu ya Pili.

Katika ziara hiyo, Kamati ya Bunge iliipongeza TAEC kwa hatua kubwa iliyofikia katika utekelezaji wa ujenzi wa mradi huo unaojengwa na Serikali kwa jumla ya kiasi cha shilingi Billioni 10.4.
Akitoa taarifa ya mradi kwa Kamati ya Bunge Mkurugenzi Mkuu wa TAEC, Profesa Lazaro Busagala alisema awali TAEC iliingia mkataba na Wakala wa Ujenzi Tanzania (TBA) kwa ajili ya ujenzi wa maabara awamu ya kwanza Mei 29, 2017.

Ujenzi rasmi wa Maabara Changamano awamu ya kwanza uliaanza Juni Mosi, 2017, ambapo ulikamilika kwa kiasi cha shilingi billioni 2.3 na kuzinduliwa rasmi na Mheshimiwa Kassim M. Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 29 Aprili 2018.
Ujenzi wa Maabara ya Awamu ya pili unahusisha Maabara zifuatazo; i. Maabara ya kupima mionzi ya Alpha (Alpha Spectrometry Laboratory); ii. Maabara ya kupima mionzi ya Beta (Beta Counting Laboratory); ya kupima mionzi ya Gamma (Gamma Spectrometry Laboratory); iii. Maabara ya kupima mionzi kwenye damu (Cytogenetic Laboratory);

iv. Maabara ya kupima viwango vya metali kwenye sampuli (X-Ray Fluorescence Laboratory); 4 v. Maabara ya kufanya matengenezo ya vifaa vya mionzi (Nuclear Instrumentation and Maintanance Laboratory); vi. Maabara ya uandaaji wa sampuli kikemikali (Radiochemistry Laboratory); vii. Maabara ya kufanyia matengenezo mabaki ya vyanzo vya mionzi (Radioactive Wastes Conditioning Laboratory).
Profesa Busagala alisema kuwa, hadi kufikia Machi 9, 2022, hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa Maabara Changamana Awamu ya Pili (mradi namba 6352) ujenzi ulikuwa umefikia asilimia 94 ambapo upo mbele kwa miezi mitatu ukilinganisha na mpango kazi (work program) uliokuwa umepangwa kwenye mkataba.

Akimalizia taarifa yake Profesa Lazaro aliishukuru Kamati ya Bunge na kutoa shukrani za dhati kwa Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kuendelea kuisimamia, kuitegemeza na kuiwezesha TAEC katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo huku akiiomba Serikali iendelea kuiwezesha taasisi kufikia malengo yake kwa manufaa ya jamii ya Watanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news