Utabiri wa hali ya hewa kwa saa 24 zijazo

UTABIRI wa hali ya hewa usiku wa leo Machi 4,2022 (kwa saa 24 kuanzia saa tatu usiku) hadi Machi 5,2022 unaletwa kwenu na Mchambuzi kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Bi.Tabu Kwedilima.

Mikoa ya Kagera, Geita, Lindi, Ruvuma, Mtwara, Kigoma, Tabora, Katavi, Rukwa, Songwe, Iringa, Mbeya na Njombe matarajio ni mvua na ngurumo katika maeneo machache na jua. Huku mikoa ya Morogoro, Dodoma na Singida matarajio ni mvua na vipindi vya jua.

Kwa upande wa Dar es Salaam na Pwani ikijumuisha visiwa vya Mafia matarajio ni mvua nyepesi na jua.

Aidha, Tanga, Visiwa vya Unguja na Pemba, Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara matarajio ni vipindi vya jua

UPEPO WA PWANI:

Unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya km 30 kwa saa kwa Pwani yote kutoka Kaskazini Mashariki kwa Pwani ya Kaskazini, na kutoka Mashariki kwa Pwani ya Kusini.

Pia kwa mujibu wa TMA, hali ya bahari mawimbi makubwa kiasi huku yakitarajiwa mabadiliko kidogo Machi 6, 2022.

VIWANGO VYA JOTO, MAWIO NA MACHWEO YA JUA KWA BAADHI YA MIJI HAPA NCHINI:

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news