Utabiri wa hali ya hewa Saa 24 zijazo/Next 24 Hours Weather Forecast

*MVUA NA NGURUMO INATARAJIWA KATIKA BAADHI YA MAENEO YA NCHI

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

UTABIRI wa hali ya hewa saa 24 zijazo kuanzia saa tatu usiku wa leo Machi 23,2022 mchambuzi ni Akili Mwangaza kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Hali ya Bahari: Inatarajiwa kuwa na mawimbi makubwa kiasi huku matarajio kwa siku ya Ijumaa ya Machi 25,2022 ni mabadiliko kidogo.


Kwa mujibu wa TMA, hali ya hewa SAA 24 zijazo kuna matarajio ya mvua na ngurumo kwa baadhi ya maeneo ya Ziwa Victoria, Magharibi na Nyanda za Juu Kusini

Mikoa ya Ruvuma, Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu, Morogoro, Kigoma, Katavi, Tabora, Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa, Njombe, Lindi, Mtwara, Tanga, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia) pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.

Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.

Mikoa ya Dodoma na Singida inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.

Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya kilomita 30 kwa saa kwa Pwani yote kutoka Kusini kwa Pwani ya Kaskazini na kutoka Kusini Mashariki kwa Pwani ya Kusini.

TANZANIA WEATHER FORECAST 23/03/2022:THUNDERSHOWERS IS EXPECTED OVER SOME AREAS OF THE COUNTRY.

Weather forecast for the next 24 hours starting 21:00 tonight 23.03.2022 as presented by weather analyst Mohamed Hamis from Tanzania Meteorological Authority (TMA).

Post a Comment

0 Comments