Utabiri wa hali ya hewa Tanzania saa 24 zijazo/ Weather Forecast for the next 24hours

UTABIRI wa hali ya hewa saa 24 zijazo kuanzia leo saa 3 usiku wa Machi 15, 2022 unaletwa na mchambuzi, Noel Mlay kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).Hali ya Bahari: Inatarajiwa kuwa na Mawimbi madogo hadi makubwa kiasi huku matarajio kwa siku ya Alhamisi ya tarehe 17/03/2022 yakitarajiwa mabadiliko kidogo.

Kwa mujibu wa TMA, saa 24 zijazo maeneo ya Pwani ya Kaskazini na Nyanda za Juu Kaskazini yanatarajiwa kuendelea kuwa makavu.

Mikoa ya Ruvuma, Kagera, Geita, Mwanza, Mara, Shinyanga, Simiyu, Kusini mwa Mkoa wa Morogoro,Dodoma, Singida, Kigoma, Katavi, Tabora, Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa na Njombe inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.

Mikoa ya Lindi, Mtwara na Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua katika maeneo machache na vipindi vya jua.

Visiwa vya Unguja na Pemba, Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia): inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.

Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya kilomita 30 kwa saa kutoka Kaskazini Mashariki kwa Pwani ya Kaskazini na kwa kasi ya kilomita 20 kwa saa kutoka Kaskazini kwa Pwani ya Kusini.
 

TANZANIA WEATHER FORECAST 15/03/2022

THUNDERSHOWERS ARE EXPECTED OVER GEITA, KAGERA, TABORA, KIGOMA, KATAVI, RUKWA, MBEYA, SONGWE, MOROGORO(KUSINI), IRINGA, NJOMBE AND RUVUMA REGIONS.

Weather forecast for the next 24 hours starting tonight at 9:00 p.m on 15-03-2022 as presented by weather analyst Godfrey Kazinja from Tanzania Meteorological Authority (TMA).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news