Utabiri wa hali ya hewa Tanzania saa 24 zijazo/Next 24 hours Weather forecast

>MAWINGU, MVUA NA NGURUMO VINATARAJIWA KWA BAADHI YA MAENEO YA MIKOA YA RUKWA, MBEYA, SONGWE, IRINGA, NJOMBE NA RUVUMA

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

UTABIRI wa hali ya hewa wa saa 24 kuanzia saa tatu usiku wa leo Machi 19,2022 unaletwa na mchambuzi, Daniel Masunga kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Huku maeneo ya Nyanda za Juu Kaskazini na maeneo machache ya Pwani ya Kaskazini yakitarajiwa kuwa na mvua nyepesi baada ya kuwa makavu kwa kipindi.

Aidha, mikoa ya Ruvuma, Kusini mwa Mkoa wa Morogoro, Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa na Njombe inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vifupi vya jua

Mikoa ya Dodoma, Singida, Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro, Kigoma, Tabora, Katavi, Kagera, Mwanza, Geita, Shinyanga, Lindi na Mtwara inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.

Kwa muibu wa TMA, mikoa ya Dar es Salaam, Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Pwani ikijumuisha visiwa vya Mafia inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.

Mikoa ya Mara na Simiyu inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.

Visiwa vya Unguja na Pemba, Mkoa wa Tanga inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.

Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya kilomita 20 kwa saa kwa Pwani yote kutoka Kaskazini Mashariki kwa Pwani ya Kaskazini na kutoka Kaskazini kwa Pwani ya Kusini.

Hali ya Bahari: Inatarajiwa kuwa na mawimbi madogo ambapo matarajio kwa siku ya Jumatatu ya tarehe 21, Machi 2022 huena kukawa na mabadiliko kidogo.

TANZANIA WEATHER FORECAST 19/03/2022

CLOUD &THUNDERSHOWERS ARE EXPECTED OVER SOME AREAS OF RUKWA, MBEYA, SONGWE, IRINGA, NJOMBE AND RUVUMA REGIONS.

Weather forecast for the next 24 hours starting tonight at 9:00 p.m on 19-03-2022 as presented by weather analyst Daniel Masunga from Tanzania Meteorological Authority (TMA).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news