Utabiri wa hali ya hewa Tanzania saa 24 zijazo/Next 24 hours Weather forecast

>MVUA NA NGURUMO INATARAJIWA KATIKA BAADHI YA MAENEO YA NCHI

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

UTABIRI wa hali ya hewa saa 24 zijazo kuanzia 3:00 usiku leo Machi 22,2022 unawasilishwa na mchambuzi Noel Mlay kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Kwa mujibu wa TMA, Baadhi ya Maeneo yanatarajiwa kupata mvua zenye ngurumo za radi na maeneo machache mvua nyepesi.

Mikoa ya Ruvuma, Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Kusini mwa Mkoa wa Morogoro, Kigoma, Katavi, Tabora, Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa, Njombe, Lindi, Mtwara, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia) pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.

Aidha, mikoa ya Mara na Simiyu inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.

Mikoa ya Tanga na Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua katika maeneo machache na vipindi vya jua.

Mikoa ya Dodoma, Singida, Arusha, Manyara na Kilimanjaro inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.

Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvuma kutoka Kusini Mashariki kwa Pwani yote kwa kasi ya kilomita 30 kwa saa kwa Pwani ya Kaskazini na kwa kasi ya kilomita 20 kwa saa kwa Pwani ya Kusini.

Hali ya Bahari: Inatarajiwa kuwa na mawimbi madogo hadi makubwa kiasi ambapo matarajio kwa siku ya Alhamisi ya Machi 24,2022 huenda kukawa na mabadiliko kidogo.


TANZANIA WEATHER FORECAST 22/03/2022:THUNDERSHOWERS IS EXPECTED OVER SOME AREAS OF THE COUNTRY
Weatherforecast for the next 24 hours starting 21:00 tonight 22.03.2022 as presented by weather analyst Amina Saleh from Tanzania Meteorological Authority (TMA).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news